Diwani wa kata ya
Igombavanu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa Mh. HABIBU KILONGE amefariki Dunia katika
hospitali ya wilaya ya Mufindi usiku wa kuamkia leo ilikokuwa amelazwa kwa
matibabu.
Taarifa ya mwenyekiti
wa Halmsahauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. FESTO
MGINA kupitia kitengo cha habari na mawasiliano cha Halmashauri ya Wilaya,
ameeleza kuwa, marehemu amefarikia baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa
takribani mwezi mmoja na mara kadhaa alikuwa akitibiwa katika hospitali ya
Wilaya na kurejea nyumbani.
Aidha, amebainisha
ratiba ya shughuli za maziko kuwa marehemu atazikwa Jumapili ya Tarehe 17
ambapo mapema asubuhi ya saa mbili mwili wa marehemu utaondolewa katika Hospitali
ya Wilaya Mafinga na kupekwa katika kata ya Igombavanu ambakoa utaagwa na
wapiga kura wake na itakapofika saa tano asubuhi mwili huo utasafirishwa kwenda
Kijiji cha kichiwa Mtwango Mkoani Njombe ambako ndiko mwili huo utazikwa.
Marehemu Diwani HABIBU KILONGE alichaguliwa kwa mara ya
kwanza na wananchi wa Kata ya Igombavanu kupiti atiketi ya chama cha Mapinduzi
CCM katika uchaguzi Mkuu uliyofanyika mapema mwezi wa 10 mwaka jana kwa jumla
ya kura Elfu 2 na 34 ikiwa ni ushindi mkubwa dhidi ya mpinzani wake wa karibu
kutoka chama cha Chadema aliyepata kura 361
na mpaka mauti inakuta diwani huyo alikuwa amehudhuria kikao kimoja pekee,
ambacho kilikuwa maalu kwa kuapishwa.
0 comments:
Post a Comment