Friday, January 22, 2016

OJADACT WALAANI SHERIA YA MAGAZETI YA MWAKA 1976. WAMWOMBA MAGUFULI KUINGILIA KATI.

Mwenyekiti wa Chama hicho Edwin Soko akizungumza na Wanahabari Jijini Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo 
Chama cha Waandishi wa Habari Wanaopiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Nchini OJADACT, Kimemuomba Rais Dkt.John Pombe Magufuli kutekeleza ahadi yake ya kufanyia marekebisho sheria kandamizi kwa vyombo vya habari nchini, aliyoitoa wakati wa Kampeni zake za Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana.

Mwenyekiti wa Chama hicho Edwin Soko, ametoa ombi hilo hii leo mbele ya Wanahabari Jijini Mwanza, wakati akielezea hatua mbalimbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Serikali dhidi ya vyombo vya habari vinavyokiuka sheria katika utendaji wake wa kazi.

Soko alitolea mfano Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 kupitia sura ya 229 kifungu cha 25 (1), kinachompa Mamlaka Waziri wa Habari kulifungia gazeti lolote linalotoa habari zenye ukakasi, kuwa ni ishara ya ukandamizaji wa uhuru wa habari nchini, kwa kuwa kuwa sheria hiyo haitoi nafasi kwa chombo kinacholalamikiwa kujitetea ikizingatiwa kwamba Serikali ndiyo mlalamikaji na wakati huo huo mtoa hukumu.

“Sheria ya Magazeti ni mbaya kwani haitoi nafasi kwa upande wa pili kujibu, huku serikali ikiwa ndiyo mlalamikaji na hapo hapo hakimu (Unfair game). Alitanabaisha Soko na kuongeza kuwa OJADACT inalaani matumizi ya sheria ya magazeti nchini ya mwaka 1976.

Wakati OJADACT ikitoa ombi hilo kwa Rais Dkt.Magufuli, baadhi ya Waandishi wa Habari Jijini Mwanza walikiri kuwepo kwa sheria zenye ukandamizaji wa Uhuru wa habari nchini ambapo wameomba sheria hizo kurekebishwa ili kukuza haki ya kutafuta na kutoa habari katika jamii.

Vyombo mbalimbali vya Habari nchini hususani Magazeti, vimekuwa vikikabiliwa na sheria kadhaa ambazo zimekuwa zikilalamikiwa ya kwamba zinakiuka misingi ya uhuru wa habari ambapo ni hivi karibuni Serikali imelifungia gazeti la Mawio kuchapisha habari zake kutokana na kuchapisha taarifa zilizoelezwa kuwa na mkanganyiko katika jamii.
Mwenyekiti wa Chama hicho Edwin Soko akizungumza na Wanahabari Jijini Mwanza.
Wanahabari
Kulia ni Mmoja wa Wanahabari kutoka Jijini Mwanza akitoa maoni yake kwa kinasa sauti cha BMG

Kushoto ni Mmoja wa Wanahabari kutoka Jijini Mwanza akitoa maoni yake kwa kinasa sauti cha BMG
Kushoto ni Mmoja wa Wanahabari kutoka Jijini Mwanza akitoa maoni yake kwa kinasa sauti cha BMG
Baada ya Ojadact kutoa ombi lake kwa Mhe.Rais, Ikafuata Selfie
Kutoka Rock City Jijini Mwanza, Mimi ni GB Pazzo wa Binagi Media Group

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More