UMOJA
wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umekitaka chama hicho kumvua
uanachama Rais mstaafu wa Zanzibar Dk Aman Abeid Karume.
Kauli
hiyo ilitolewa jana katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar na
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Khamis wakati wa kilele cha
matembezi ya vijana wa umoja huo kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi.
Alimshushia
tuhuma nzito mstaafu huyo kuwa anashirikiana na wapinzani kukihujumu
chama hicho kikongwe nchini, na kwamba asipofukuzwa umoja huo utatumia
njia zingine ambazo hakuziweka wazi.
Sadifa
alionya kwamba Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar si mali wala miliki ya
mtu kwani Wazanzibar wote wana haki ya kushiriki kuyaenzi kwa vitendo
kutokana na historia yake.
0 comments:
Post a Comment