Siku
moja baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe kusema akionana na waliokuwa wanachama wa CCM
na kuhamia upinzani anajisikia kichefuchefu, waliokuwa makada wa chama
hicho wamemshukia kwa kauli yake hiyo.
Membe
alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akitoa maoni yake kuhusu makada
waliohama na kusisitiza kuwa wasipokewe endapo watataka kurudi.
Aliyekuwa
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole
Medeye ambaye alitimkia Chadema, alisema kama angesikia maneno hayo kwa
mtu mwingine asingeshangaa, lakini siyo kwa Membe.
Mbunge
huyo wa zamani wa Arumeru – Magharibi, alisema Membe anapata masilahi
yake kwa kutambulika kama waziri mstaafu na wakati anaapa kuwa katika
nafasi hiyo alitumia Katiba ambayo hivi sasa kwa kupinga yaliyomo
ikiwamo uhuru wa mtu kujiunga na chama chochote cha siasa, anakosea.
Medeye
alisema kwa kauli hiyo, Membe hana haki ya kugombea nafasi yoyote ya
siasa kwa sababu haamini katika vyama vingi wakati Taifa linaendeshwa
kwa Katiba inayokubali suala hilo.
Alisema
hata kauli ya Membe ya kutounga mkono uchaguzi kurudiwa Zanzibar
akitaka kufanyiwa kazi kasoro chache ni ya kinafiki kwa sababu
ameonyesha kutopenda upinzani.
“Hana
msimamo hazungumzi vitu kutoka moyoni, kama kweli anakubali vyama vingi
na ana uchungu na kinachoendelea Zanzibar, kwa kuwa bado ni mjumbe wa
Nec (Halmashauri Kuu ya CCM), angemuomba mwenyekiti wake aitishe mkutano
mkuu lijadiliwe hilo na atoe anachokiamini, hakufanya hivyo kwa sababu
hakubali vyama vingi, hataki mabadiliko katika siasa anayoitumikia, ” alisema Medeye.
Aliyekuwa kada mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru alisema hawezi kujibizana na watu kwani anajua anachofanya.
Alisema
anayo mawazo huru na akitaka kuzungumza jambo lolote atafanya hivyo kwa
utashi wake na siyo kujibizana na watu waliozungumza kwa utashi wao.
Aliyewahi
kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita alisema
anamheshimu Membe kwa sababu amefanya naye kazi katika chama hicho
tawala na kumshauri siku nyingine anapozungumza mambo kama hayo
asiegemee upande mmoja.
Alisema
licha ya kuwa hayo ni mawazo yake na kila mtu ana uhuru wa kuwaza na
kusema anachotaka, alipaswa apime anazungumza nini na kwa manufaa ya
nani.
Guninita
alisema Katiba ya nchi inamruhusu mtu kuhama chama hata mara 10
alimradi huko anakokwenda atapata vitu muhimu ikiwamo malengo yake
binafsi, ya chama husika na mafanikio ya Taifa.
Alisema haikuandikwa ni lazima abaki sehemu anayoamini hana malengo nayo, au asihame kutoka chama kimoja ama kingine
0 comments:
Post a Comment