Saturday, January 9, 2016

TFF KWA HILI HAMJAMTENDEA HAKI SAMATTA HATA KIDOGO







KWANINI TFF WANATAKA KUMHUJUMU SAMATTA??


By Malisa GJ,

Hii nchi kuna watu wanapaswa kufungwa au kupewa adhabu kali iwe fundisho. Miongoni mwao ni Rais wa TFF Jamal Malinzi na safu yake ya uongozi. Ningekua na mamlaka Malinzi leo angelala "Keko au Segerea"..

Mbwana Samatta ameleta HESHIMA KUBWA sana Tanzania ambayo viongozi wa kisiasa wameshindwa kutuletea kwa miaka zaidi ya 50. Ushindi wa tuzo ya Mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ni ushindi mkubwa sana kwa taifa letu. Samatta ameitangaza nchi yetu kwa kiwango kikubwa sana. Waliokua hawaijui Tanzania sasa wataijua bila kupenda.

Brother Anthony Mtaka ambaye ni mwanasiasa hodari, msomi na miongoni mwa watu wachache ndani ya CCM wanaonivutia kisiasa; amesema kuwa Samatta ametangaza Tanzania vizuri kuliko viongozi wa Serikali waliotumia mabilioni ya fedha kwa miaka kumi mfululizo (2005 -2015) kutangaza vivutio vya utalii na wakashindwa.

Ni wazi kuwa heshima aliyotupa Sammata ni kubwa sana na tunapaswa kuheshimu mchango wake hasa ukizingatia kwamba amefika hapo kwa juhudi binafsi. Sio TFF wala Serikali zilizochangia mafanikio ya Sammata. Ni yeye mwenyewe na Mungu wake.

So ilitakiwa TFF waweke utaratibu mzuri wa kumpokea Samatta kwa heshima. Ikiwezekana watu wafanye maandamano ya amani kuanzia pale Airport hadi mahali watakapokusanyika. Kama tunaandamana kwa sababu za kisiasa kwanini tusiandamane kumpongeza mtanzania mwenzetu aliyeitangaza vema nchi yetu kimataifa?

Tena ingepaswa tuwe na Media Campaign maalum ya kumpongeza Samatta. Na tufanye "hashtag" kwenye mitandao ya kijamii kama FB, Tweeter, Instagram etc. Tujenge ushawishi watu wajitokeze kwa wingi uwanja wa ndege wa JNIA hadi Samatta mwenyewe asikie fahari na ajivunie kuwa Mtanzania.

Lakini cha ajabu TFF kwa kushirikiana na CAF wameamua kumhujumu Samatta. Na serikali imekaa kimya as if nothing is gojng on. Rais wa TFF Jamal Malinzi ameandika kupitia ukurasa wake wa Tweeter kuwa Samatta atatua nchini saa 8 za usiku kesho jumamosi. Seriously?? Saa 8 usiku?? Apokelewe na "wanga" au??

Rafiki yangu Ezekiel Kamwaga amehoji kwanini isitafutwe ndege ya saa 4 asubuhi kesho ili watu waweze kujitokeza kwa wingi kumpokea? Hivi kweli hatuwezi kum-market shujaa wetu?? Kama tulishindwa kumsaidia kufika hapo alipofika, hata kumfanyia marketing tunashindwa? Hivi mnadhani Samatta angekua Mkenya angepokelewa saa 8 za usiku?? TFF kuweni serious kidogo, acheni ujinga.!

Saa 8 za usiku watu wanakoroma vitandani, wengine wako club wameshalewa "ndovu baridi" ndio mmeona ni muda mzuri wa kumpokea Sammata? Wanaopokelewa usiku wa manane ni "majambazi na wanga" sio shujaa kama Samatta.

Halafu Malinzi kwa kujishtukia anajaribu kupunguza ukali wa maneno na kusema eti Samatta atatua kesho "saa 8 alfajiri". Hakuna kitu kinachoitwa "saa 8 alfajiri" kwenye Kiswahili. Ni saa 8 usiku. Alfajiri inaanza saa 11. Sasa hiyo alfajiri ya Malinzi ya saa 8 usiku ameitoa wapi?

Pia utetezi wa Malinzi ni wa "kitoto sana". Sio utetezi wa kiongozi tena wa taasisi kubwa kama TFF. Malinzi anasema saa 8 usiku ndio muda ambao Samatta amekatiwa ticket na Shirikisho ls Soka Afrika (CAF ) ambao ndio waandaaji wa tuzo hizo. Hivi kwani kila wanachofanya CAF lazima tukubaliane nacho bila kuhoji?

Ilipaswa TFF wajiulize kwanini CAF wamemkatia Samatta ndege ya usiku wakati ndege za asubuhi au mchana zipo.?? Jibu ni rahisi tu kwamba CAF wanaendeleza juhudi zao za kuhujumu nchi za Afrika Mashariki. Hawapendi kabisa kuona nchi zetu za Afrika Mashariki zikifanikiwa kisoka. Ndio maana hata kwenye michuano ya kimataifa wamekua wakitupanga na timu ngumu kama "Ghana, Senegal, Cameroon, Algeria, Misri, Nigeria" etc ili tusifike mbali.

Kwahiyo hili la kumpangia Sammata kurudi saa 8 usiku sio bahati mbaya. Itz a planned and organized matter. Lengo lao tushindwe kumpa Samatta mapokezi mazuri na ya heshima. Kwahiyo ilitakiwa viongozi wa TFF waione hujuma hii na waikatae.

Sifa ya kiongozi ni kuona pale ambapo wengine hawawezi kuona (A Leader must be able to see where others cannot see). So TFF walitakiwa waone kuwa muda aliopangiwa Sammata (saa 8 usiku) ni hujuma za CAF, then wafikirie mbinu mbadala ya kukataa hujuma hiyo. Ikiwezekana kumfanyia booking upya Samatta ili atue nchini Asubuhi, Mchana au jioni muda ambao watu wengi wanaweza kujitokeza kumpokea.

Lakini viongozi wa TFF wanakaa na vitambi vyao vya "Castle lite" wanakubaliana tu na CAF bila hata kureason kidogo. Huu ni ujinga ambao hata Mwenyekiti wa "wajinga duniani" hawezi kufanya.

Ingekua Samatta ni MKenya; kwanza wangekataa hiyo ticket ya CAF ya saa 8 usiku. Then wangemfanyia booking upya Samatta kwa pesa zao ili aweze kutua kwa muda wanaotaka wao. Na ingewezekana wangemtumia hata ndege maalumu ya kwenda kumchukua.

Lakini hapa bongo TFF wamekaa tu kama "mazuzu" wanakimbilia kuandika Tweeter bila aibu eti Samatta atatua kesho saa 8 usiku. Nani akampokee saa 8 usiku?? Labda Malinzi na familia yake.

MY TAKE.!
Natoa wito kwa watumiaji wote wa mitandaoTushikamane kwa umoja wetu bila kujali vyama vyetu, dini, kabila au timu tunazoshabikia, tupige kelele mitandaoni kuhakikisha Samatta anatua nchini muda ambao watanzania tunaweza kwenda kumpokea.

Kama itakosekana ndege ya kesho mchana bora aje Jumapili asubuhi kuliko kuja hiyo kesho saa 8 usiku. Share ujumbe huu, mtag kiongozi yeyote wa Serikali au wa TFF. Kama una namba zao wapigie au watumie sms kuonesha kulaani hujuma inayotaka kufanywa dhidi ya Sammata ya kumpokea saa 8 za usiku. Natoa wito pia kwa Serikali iingilie kati suala hili. Mpigieni #Nappemwambieni hatuko tayari kumpokea Samatta saa 8 za usiku.


Tunamtaka Sammata muda ambao tunaweza kumpokea sio saa 8 za usiku.#JUSTICE_4_SAMMATA.!

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More