Saturday, January 30, 2016

Wanamauzo 4,760 wapewa elimu ya ujasiriamali na Tigo

Baadhi ya wanamauzo wa kanda ya pwani ya Tigo wakiwa katika picha ya pamoja siku ya mahafali yao ya kuhitimu mafunzo maalum ya ujasiriamali yaliyotolewa na Tigo

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

jitihada za kuwawezesha wafanyakazi wake wa kujitegemea kumudu changamoto mbalimbali za kikazi na kimaisha, Tigo imewapa wafanyakazi hao wapatao 4,767 mafunzo maalum ya ujasiriamali kupitia mpango wake wa mafunzo kazini.

Mpango wa Tigo wa mafunzo kazini kwa wanamauzo wakujitegemea uitwayo Tigo Sales School (TSS) ulianzishwa mwaka 2012 ambapo kwa mujibu wa Meneja wa TSS Justine Kwizera, kampuni inatarajia kutoa mafunzo hayo kwa wanamauzo wake wote wapatao 10,000 katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Alisema kila mwaka Tigo huwekeza kiasi cha 600m/- katika mpango huu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kampuni hiyo wa kuimarisha utoaji huduma kwa wateja wake. Tigo ina zaidi wateja milioni kumi.

“Mpango wa TSS unalenga katika kuwajengea uwezo wa kiutendaji kazini wanamauzo wa kujitegemea wa Tigo pamoja kuwapa mbinu za kujikimu katika kukabiliana na changamoto mbalimbali maishani,”amesema Kwizera katika mahojiano maalum.

Mafunzo yanayotolewa na TSS ni pamoja na stadi za mauzo, ujasiriamali, usimamizi wa fedha na huduma kwa wateja, alisema Kwizera na kuongeza kwamba mafunzo hudumu kwa muda wa siku nane darasani  na kufuatiwa na mafunzo kwa vitendo kwa miezi mitatu.

“Mafanikio ambayo tumeyashuhudia kutokana na mafunzo haya ni ongezeko kubwa la mauzo na kuimarika kwa huduma kwa wateja sambamba na mabadiliko chanya katika hali ya maisha ya wanamauzo wetu,” alisema meneja huyo wa TSS.

Aidha alisema Tigo inaendeleza kutoa mafunzo kwa wanamauzo katika kila duka na ofisi zake 24 za mauzo  nchi nzima ili kuendeleza watendaji wakezaidi.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More