MAHAKAMA
ya wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemhukumu mkazi wa Mtaa wa Mpanda
Hoteli, Manispaa ya Mpanda, Frank Jonas (27) kutumikia kifungo cha miaka
30 jela kwa kosa la kutaka kumbaka binti wa miaka 17 .
Hukumu hiyo ilitolewa Ijumaa iliyopita na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Chiganga Ntengwa.
Baada
ya hukumu hiyo, baadhi ya watu walioshuhudia hukumu hiyo walihamasika
na kudai hawakujua kama kosa la kutaka kubaka linaweza kumfunga mtu
miaka 30 jela.
Hakimu Ntengwa alitoa hukumu hiyo baada ya mshtakiwa kukiri kutenda kosa lake hilo.
Awali,
kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo Mwendesha Mashitaka wa Serikali,
Ongela Malifimbo, alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari 9,
mwaka huu, saa 8:00 mchana katika eneo la shule ya Sekondari Mwangaza
mjini Mpanda.
Ilidaiwa
siku ya tukio mshtakiwa alimvizia msichana huyo wakati alipokuwa
akipita katika eneo hilo kisha akamburuta kwenye nyasi ndefu kwa nia ya
kumbaka.
Mwendesha
Mashitaka huyo, alieleza mahakamani hapo kuwa baada ya kumburuza mpenzi
wake huyo kwenye nyasi hizo ndefu, alimchojoa kwa nguvu nguo zake,
kisha alimlalia juu ya kifua chake huku msichana huyo akipiga mayowe ya
kuomba msaada.
Alieleza
watu waliokuwa karibu na eneo hilo baada ya kuwa wamesikia mayowe hayo
na walifika kwenye eneo hilo la tukio, ambapo walikuta Jonas akiwa
amemlalia kifuani msichana huyo huku akihangaika kumchojoa nguo za
ndani.
Ilidaiwa
kuwa watu hao, walilazimika kumchomoa kwa nguvu juu ya kifua cha
msichana huyo huku mtuhumiwa akiwa anawasihi wamuachie kwani anamfanyia
hivyo kwa vile ni mpenzi wake ambaye alikuwa amekula fedha zake.
Hata
hivyo, walimwondoa kwa nguvu kumpeleka kwenye kituo cha Polisi cha
Mpanda huku akiwa hajatimiza lengo lake la kumbaka msichana huyo. Katika
utetezi wake mshitakiwa aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa
alifanya hivyo kwa vile msichana huyo alikuwa ni mpenzi wake na alikuwa
amekula fedha zake.
Maombi
hayo yalipingwa na mwanasheria wa Serikali kwa kile alichodai kuwa hata
kama alikuwa ni mpenzi wake hakutakiwa kutaka kumbaka.
0 comments:
Post a Comment