DR MSEKWA AKIWAONYESHA WAANDISHI WA HABARI KUTOKA NURU FM GERLAD MALEKELA NA DENIS NYALI ENEO LA KUNYWESHA MAJI MIFUGO YAKE
NA FREDY MGUNDA,IRINGA
Idara ya kilimo mkoani
iringa imeshauriwa kuwatembea wakulima wadogo wadogo ili kujua maendeleo yao na
kutoa ushauri wa kilimo bora.
Akizungumza na blog hii Dr
msekwa ambaye ni mganga wa tiba asili na mtafiti wa kilimo na ufugaji katika
kijiji cha tanangozi wilaya ya iringa amesema yeye pamoja na mkewe waliweza
kuusaidia mkoa wa iringa kushika nafasi ya kwanza kwenye maadhimisho ya nane yaliyofanyika mkoani
mbeya na kupata zawadi ya shilingi
milioni mbili kama wafugaji bora wa kuku wa kienyeji.
Dr msekwa anasema alitarajia
viongozi na wataalamu wangemtembelea ili kumtia moyo na kumpa njia nyingine za
uzalishaji bora wa kilimo na ufugaji.
Lakini hali imekuwa tofauti toka amepata
ushindi huo hajawahi kupata ushauri wowote wa kilimo kutoka idara yoyote ya kilimo
wala mtaalam yeyote Yule aliyewahi kufika katika eneo analofanyia shughuri za kilimo na ufugaji.
Dr msekwa ni mganga wa tiba
za asili, mkulima ,na mfugaji anayeishi
katika kijiji cha tanangozi wilaya ya iringa amekuwa akijishughurisha na
ufugaji wa kuku wa kienyeji,ng’ombe wa maziwa na kuku wa mayai pamoja kilimo
cha nyanya,mahindi,maharage na mazao mengine yote ya kilimo.
DR huyu ambaye pia ni Mkulima
amekuwa na msaada mkubwa kwa wananchi wanaomzunguka kwa kutoa msaada wa vifaa
mbalimbali vya kilmo pamoja na ushauri mbalimbali juu ya kilimo kwa kuwa
anataaluma ya kilimo.
Aidha anasikitishwa na idara
ya kilimo mkoani iringa kwa kutowatembelea wakulima wadogo kwa kuwa mara nyingi
ndio wamekuwa msaada mkubwa wa mkoa katika sherehe na mazimisho mbalimbali ya
kitaifa.
“Tulishinda zawadi ya
shilingi milioni mbili kwa kushika nafasi ya kwanza na kuupa heshima mkoa wa
iringa lakini viongozi wamekuwa hawaudhamini mchango wetu” alisema dr msekwa.
Dr msekwa amemalizia kwa
kuwaomba viongozi wa mkao wa iringa wanaohusika na masuala ya kilimo kutenga
muda na kuwatembelea wakulima ili kubadilishana mawazo na kuwapa ushauri wa
kitaalamu na kugeuza kilimo kuwa biashara.
0 comments:
Post a Comment