NA RAYMOND MINJA
IRINGA.
Jeshi la
Polisi Mkoani Iringa kwa kushirikiana na Jeshi la uhamiaji
lilinawashikiria watu 11katia yao wahamiaji haramu 8 raia wa Ephiopia kwa
kuingia nchini bila kibali.
Katika tukio hilo
watanzania watatu wakiwamo dereva na msaidizi wake wa gari la kukodi
linalotumika kusafirisha magazeti yanayochapishwa na kampuni ya Mwananchi
Communications Ltd na mtu mmoja liyejitambulisha kuw a ni msindikizaji
wanashilikiwa na jeshi hilo kwa kushiriki kusafirishwa watuhumiwa hao.
Akizungumza na
Waandishi wa habari mjini hapa jana Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Peter Kakamba
alisema watuhumiwa hao walikamtwa kwenye kituo cha ukaguzi cha Polisi cha
Igumbilo.
“Ndugu zangu leo
(jana) majira ya saa 11 alfajiri katika eneo la kizuizi cha Polisi cha ukaguzi
wa magari Igumbilo (Chek Point) ndani ya Manispaa ya Iringa,Polisi katika
ukaguzi wa kukagua magari walilikamata gari hiyo aina ya Toyota Hiace yenye
namba za usaliji T.745 DED.likiwa limepakia magazeti ya Mwananchi na wahamiaji
kutoka Ephiopia 8”alisema Kakamba
Aliwataja madeva
waliokuwa wakiendesha gari hilo kuwa ni Godfrey Kaka 32)akiwa na masaidizi wake
Michael Jafet (37) wote wakazi wa Jijini Dar es Salaam na mtu mmoja
aliyefahamika kwa Elias Patson mkazi wa Jijini Dar es Salaam aliyedai alikuwa
msindikizaji.
“Bado haijafamika
kama huyu aliyejitambulisha kuwa ni msindikizaji alikuwa asindikiza wahamiaji
haramu ama magazeti na Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi juu ya jambo
hili”alisema Kakamba.
Kakamba alifafanua
kuwa mara jeshi litakapomaliza kazi ya uchunguzi na kwa kushirikiana na jeshi
la uhamiaji watawafikisha watuhumiwa hao mahakamani kujibu shitaka lao.
Alionya kuwa
oparesheni ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu yakiwamo makosa mbalimbali
pamoja na wahamiaji haramu itaendelea hadi hapo watakapohakikisha vitendo hivyo
havijirudii.
Naye Mmoja wa
watuhumiwa hao ambaye ni dereva wa gari lililotumika kusafirisha magazeti hayo
Michael Jafet alisema waliwapakia wahamaiaji hao eneo la Mbezi jijini Dar
es Salaam.
“Sisi tulipokuwa
tukiondoka jana majira ya saa nane usiku kwenye makoa makuu ya Ofisi za
Mwananchi Communications Ltd na tulipofika eneo la Mbezi mtu mmoja ambaye
hatumfahamu alisimamisha gari na kutuomba tuwapakie watu hawa akitutaka
tuwashushe eneo la Nyololo mkoani hapa”alisema Jafet.
Alifafanua kuwa
kila mtu katia yahao walioapanda waliwalipa Sh 30,000 kama nauli ya kutoka Dar
es Salaam hadi Nyololo mkoani Iringa.
Tukio hilo
limekuja wakati kasi ya kukamatwa kwa watuhumiwa wanaoingia nchini kinyume na
sheria ikizidi kuongezeka kila uchao.
Januari 16 mwaka
huu katika eneo la Mahenge kata ya Mazombe wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa
Polisi walikamata watuhumiwa 85 kati yao wahamiaji haramu kutoka Ephiopia
wakiwa 83,na jana watuhumiwa 11 raia kutoka Ephiopia wakiwa nane.
Hatua hiyo
imefanya jeshi la Polisi Mkoani Iringa kuwashikilia watu walioingia nchini
kinyume na sheria kufikia 91katika kipindi cha mwezi januaria pekee.
0 comments:
Post a Comment