Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akipanda miti jana wilayani
humo ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti. Benki ya
Diamond Trust Tanzania imedhamini shughuli hiyo kwa kuchangia sh.
milioni tano. Picha kwa hisani ya DTB.
BENKI
ya Diamond Trust Tanzania, imedhamini shughuli ya upandaji miti katika
Wilaya ya Iringa iliyopo mkoani Iringa kwa kuchangia sh. milioni tano.
Wilaya ya Iringa imeanza rasmi kupanda miti katika maeneo yaliyotengwa
na uongozi wa wilaya, ikiwa ni utekelezaji wa programu ya kitaifa ya
kupanda na kutunza mazingira inayoanza mwezi huu.
Wilaya
ya Iringa inategemea kupanda zaidi ya miti 5,000 ya mbao, mapambo,
kivuli na matunda. Programu ya kupanda miti na kutunza mazingira
ilizinduliwa rasmi na Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof. Jumanne
Maghembe, wiki iliyopita.
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakati akizindua kampeni ya
kupanda miti jana alieleza kuwa, Wilaya ya Iringa imetenga maeneo
makubwa ya hifadhi ya misitu na mazingira ili kuhifadhi na kuongeza
kiwango cha maji nchini katika tarafa za Mlolo, Ismani, Kalenga, Pawaga
na Idodo.
Pia
alisisitiza umuhimu wa miti na misitu katika kuhifadhi maji na umuhimu
wa maji kwa viumbe hai. Alisema, upandaji miti na utunzaji wake
utasaidia kupata hewa nzuri, maji, mvua, kupunguza joto na kupambana na
mabiliko ya tabianchi.
Programu
hiyo ya kitaifa ni ya aina yake nchini na inashirikisha serikali kuu,
wananchi na sekta binafsi. Akizungumza na waandishi wa habari
walioshiriki katika shughuli ya kupanda miti, Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Diamond Trust Tanzania, Ndugu Viju Cherian, alisisitiza umuhimu
wa programu ya kupanda miti.
Kutunza
mazingira ni moja ya nguzo kuu ya benki yetu katika maeneo tunakofanya
biashara. Kwa kuzingatia hilo, tumeitikia wito wa Mkuu wa Wilaya na
kuunga mkono programu hii kwa kuchangia shilingi milioni tano. Benki ya
DTB ni mshirika mkubwa katika hifadhi ya mazingira nchini kote,รถ
alisema.
Benki
ya DTB ilifungua tawi katika mji wa Iringa mwaka 2014 na hadi sasa ina
matawi 24, matawi 10 yakiwa katika jiji la Dar es Salaam (tawi kuu la
Dar es Salaam Mtaa wa Jamaat, Masaki, Morocco,Magomeni, Mbezi,
Mbagala,Barabara ya Nyerere, Kariakoo, Barabara ya Nelson Mandela karibu
na njia kuu ya Tabata na Upanga katika Barabara ya Umoja wa Mataifa.
Pia
ina matawi katika miji ya Arusha, Mwanza, Zanzibar, Dodoma, Tanga,
Mbeya, Moshi, Iringa, Morogoro, Tabora, Kahama na Mtwara. Aidha, DTB ni
mshirika wa Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Aga Khan, ambao ni sehemu
ya mtandao wa maendeleo wa Aga Khan (Aga Khan Development Network).
Katika
hatua nyingine, Benki ya Diamond Trust ina matawi zaidi ya 115 katika
nchi za Afrika Mashariki ambayo inaundwa na Kenya, Tanzania, Uganda
ikiwemo Burundi.
0 comments:
Post a Comment