SHIRIKA
la Umeme (Tanesco) limetoa angalizo kwa wanaoendesha shughuli za
kilimo, kwa kuwaambia hawatakiwi kulima karibu na nguzo kwani wanapaswa
kuacha meta 30 kila upande.
Meneja
wa Tanesco wa Mkoa wa Shinyanga, Mathias Solongo alitoa angalizo hilo
kutokana na kuwapo malalamiko ya wananchi zaidi ya 50 wa kijiji cha
Seseko kata ya Mwamalili manispaa ya Shinyanga, dhidi ya Tanesco
kuwakatia mazao.
Alisema
wananchi hawaruhusiwi kulima sehemu zilizo karibu na nguzo za umeme
ikizingatiwa kwamba, walishalipwa na manispaa hakuna sehemu ambayo
haijalipwa.
“Na
inayotakiwa kulipa ni manispaa siyo shirika na tayari ilishawalipa na
katika nguzo hizo wananchi kweli hawatakiwi kulima, wanatakiwa kuacha
mita 30 kila upande lakini tofauti ya hapo haitakiwi,” alisema.
Akizungumzia
wananchi hao wanaolalamikia shirika, Solongo alishauri viongozi wa
wananchi waende kwake azungumze na kuwaelewesha vizuri suala hilo.
Awali,
wakizungumza na waandishi wa habari, wananchi hao wa kijiji cha Seseko,
kata ya Mwamalili walisema miaka yote walikuwa wakiendelea kulima na
hawakuwa na taarifa ya kuwakataza.
“Sisi
tunachohitaji ni kulipwa mazao yetu yaliyokatwakatwa ambayo yamekatwa
kimakosa kwani hata yakiiva hayafiki kwenye nguzo za umeme, baada ya
hapo tulipwe fidia yetu ya ardhi kwani bado hatujalipwa.
“Wamekata mtama wangu na mahindi yangu nitakula nini na watoto wangu, halafu wamekata bila hata kunitaarifu,” alisema William Deus.
0 comments:
Post a Comment