Wanajeshi wa Kenya
waliojeruhiwa kwenye shambulio lililofanywa na wapiganaji wa al shabaab
katika eneo la el adde wamesafirishwa hadi Nairobi.
Wapiganaji hao wa Al shabaab walishambulia kambi ya jeshi la
umoja wa mataifa nchini Somalia na kuna ripoti kuwa wanajeshi kadhaa wa
Kenya waliuawa huku wengine wakijeruhiwa.
Idadi ya wanajeshi
waliouawa haijabainika wazi lakini kundi hilo la Al shabaab linadai kuwa
liliwauwa zaidi ya wanajeshi sitini madai ambayo serikali ya Kenya
imekanusha.
Aidha
amesema wanajeshi wa Kenya bado wangali wanapambana na wapiganaji hao
wa Al shabaab ili kujaribu kuwakomboa wanajeshi waliokwama ikiwa wapo.
Kenya imekariri kuwa haitaondoa wanajeshi wake
Somalia hadi pale kundi hilo la al shabaab litakaposambaratishwa kabisa
na amani kurejea nchini humo.
Wakati huo huo kundi hilo limedai kuwa linawashikilia wanajeshi kadhaa wa Kenya mateka.
Al Shabaab limesema ni mara ya kwanza kikosi chake maalum cha Saleh ali saleh Nabhan kilifanya shambulio ndani ya somalia.
Saleh ali Saleh Nabhan alikuwa kiongozia wa Al qaeda
katika kanda ya Afrika mashariki na aliuawa kwenye shambulio
lililofanywa na Marekani mwaka wa 2008
Tangu mwaka wa 2011 wakati
Kenya ilituma wanajeshi wake nchini Somalia, kundi hilo limefanya
mashambulio kadhaa ya kigaidi nchini Kenya na kusababisha maafa makubw
0 comments:
Post a Comment