Friday, January 26, 2018

RC MASENZA AIPONGEZA TASAF KWA KAZI NZURI WANAYOIFANYA KWA WANANCHI

  Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa katika ziara ya kukagua miradi inayofanywa na wanufaika wa Mfuko wa kusaidia kaya masikini (TASAF) akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdalah na viongozi wengine wa halshauri ya wilaya ya Kilolo
 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa katika ziara ya kukagua miradi inayofanywa na wanufaika wa Mfuko wa kusaidia kaya masikini (TASAF) wakiwa kwenye moja ya nyumba ya mnufaika upande wa kushoto ndio nyumba mpya iliyojengwa na upande wa kulia nyumba ambayo mnufaika anaishi
Nyumba ya kushoto inayoonekana ndio nyumba inajengwa na mnufaika na hii ya kulia ndio nyumba anayoishi mnufaika wa TASAF wilayani kilolo
 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa katika ziara ya kukagua miradi inayofanywa na wanufaika wa Mfuko wa kusaidia kaya masikini (TASAF) akiwa kwa mnufaika wa TASAF kukagua anafanya nini baada ya kupata pesa za TASAF 
 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa katika ziara ya kukagua miradi inayofanywa na wanufaika wa Mfuko wa kusaidia kaya masikini (TASAF) akiwa kwenye moja ya nyumba za mnufaika wa TASAF 
 Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa katika ziara ya kukagua miradi inayofanywa na wanufaika wa Mfuko wa kusaidia kaya masikini (TASAF) akiwa na viongozi wa wilaya ya Mufindi wakati wa kuwa tembelea wananchi wanaonufaika na mfuko wa TASAF
 Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilya ya Mufundi Daud Yassin alikuwepo kwenye ziara ya kukagua miradi ya TASAF jinsi gani inawanufaisha wananchi 
Nyumba ya juu ndio nyumba iliyojengwa kwa kutumia pesa za mfuko wa TASAF na nyumba ya chini ndio nyumba aliyokuwa anaishi mnufaika wa TASAF 

Na Fredy Mgunda, Iringa.

MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amemaliza ziara ya kukagua miradi inayofanywa na wanufaika wa Mfuko wa kusaidia kaya masikini (TASAF) kwa kujionea changamoto zilizopo na mafaikio makubwa ambayo wanufaida wamepata katika wilaya zote za mkoa wa Iringa.

Akizungumza wakati wa ziara hizo Masenza aliwapongeza wanufaika kwa juhudi kubwa wanazozifanya kuhakikisha kuwa wanatumia vizuri pesa wanazipata kwa kufanyia vitu vya kimaendeleo.

“Nimeona juhudi zenu za kazi mnavyofanya na nimeamini kuwa TASAF imeinua maisha ya wananchi walikuwa na kipato cha chini na imani yangu kuwa biashara mnazozifanya zitakuwa na faida hapo baadae” alisema Masenza

Masenza aliongeza kuwa wanufaika wa TASAF wamejenga nyumba nzuri tofauti na walipokuwa wanaishi hapo awali naomba juhudi hizo ziendelee maana hapo watakuwa wamejiokoa kwenye swala la kuwa na makazi bora tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

“Jamini kweli maisha ya wanufaika yanabadilika angalia nyumba walikuwa wanaishi awali nah ii ya sasa hapa ndio ambapo hata Rais wetu akiona hivi atafurahi sana maana anaona matunda ya pesa anayoitoa kwa wananchi wake” alisema masenza

Aidha Masenza aliwapongeza wanufaika wote ambao wanafuga mifugo mbalimbali ya kibiashara kwa kuwa hiyo inatakuwa njia mbadala kwa maisha ya baadae hasa kipindi ambacho serikali itaacha kuttoa tena hizo pesa.

“Nawaomba endeleeni kufanya biashara,kulima na kufuga hiyo itakuwa njia nzuri ya kujiongezea kipata kwa maisha yenu na vizazi vyenu hivyo msikate taama kabisa kina mtu anaanzia chini na kwenda juu hivyo naomba mpambane kuhakikisha mnaishi maisha bora” alisema Masenza

Lakini Masenza aliwataka wataalam kufika kwa wanufaika na kuwapa elimu ya juu miradi wanayoifanya ya kimaendeleo kwa ajili ya kuboresha kipata cha kaya yao.

Nao wanufaika wa mfuko wa kusaidia kaya masikini (TASAF) mkoani iringa wameipongeza serikali kwa kuinua maisha kwa kuendelea kuwasaidia kwa kuwapa elimu ya ujasiliamali na kujua kutuzitumia vizuri pesa wanazozipata kwa kufanyia biashara.

Wakizungumza na blog hii wanufaika wa TASAF wamesema kuwa pesa ya TASAF imewasidia kufanya biashara mbalimbali ambazo zimewasidia kujikwamua kiuchumi
Nao baadhi ya wanafunzi wanaonufaika na TASAF  wameishukuru serikali kwa kufanikisha kuwasomesha kwa kupata mahitaji yote yanayohitajika shuleni.

MASENZA amewataka wanufaika kuitumia vizuri pesa wanayoipata kutoka TASAF kwa kuifanyia biashara kwa faida ya maisha ya baadae.


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More