Tuesday, January 16, 2018

MNEC SALIM ASAS AMEANZA KUIJENGA KIHESA MPYA KWA KUTEKELEZA AHADI ZAKE

 Diwani wa Kata ya Kihesa Jully Sawani  akiwa ametoka kuchukua mifuko miambili kutoka kwa MNEC Salim Asas kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Kihesa na hiyo ni baadhi tu ya mifuko ya safuri huku mingine ikiwa tayari imeshatangulia shuleni kuanza Nazi.
 Mafundi wakiwa kazini kihakikisha jengo hilo linakamilika mapema ili lianze kufanya kazi na hiyo nayo ni kazi ya MNEC Salim Asas 
 Diwani wa Kata ya Kihesa Jully Sawani akiwa katika jengo linamaliziwa kwa ufadhili wa MNEC Salim Asas 


Na Fredy Mgunda,Iringa.

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas ameanza mara moja kutekeleza ahadi zake alizowahidi wakazi wa kata ya Kihesa wakati wa kupokea hati ya diwani wa chama cha mapinduzi (CCM) wa kata hiyo Jully Sawani.

Akizungumza kwa niaba ya MNEC huyo diwani wa kata ya Kihesa Sawani alisema kuwa toka siku ya jana wameanza kufanya shughuli za kimaendeleo za wananchi kama ilivyokuwa ahadi yake na ya MNEC

“Mwandishi ukiangalia hapa unawaona mafundi wanaendeleoa na kazi hivyo najua baada ya muda mufupi kila kitu kitakuwa kimemalizika na kuanza kutumika kwa faida ya wananchi wa kata ya kihesa” alisema Sawani

Sawani alisema kuwa anamshukuru MNEC Salim Asas kwa kutekeleza ahadi alizowahidi wakazi wa kihesa kwa kuwa tayari ameshatoa mifuko mia mbili (200) ya saruji katika shule ya sekondari ya Kihesa na tayari mafundi wapo kazini wameanza kumalizia ujenzi wa jengo la biashara ambalo litaongeza ajira kwa wakazi wa kata ya Kihesa na nje ya kata hii.

“Hii unayina hapa ni saruji ambayo imetolewa na Salim Asas na hapa pia unawaona mafundi wanaendelea na kazi hivyo kazi hii inakwenda kwa kasi ili kutoa fusa ya ajira mapema iwezekanavyo na kupuza jamii tegemezi” alisema Sawani

Sawani aliongeza kuwa kazi ya kukarabati miundombinu ya barabara katika mtaa wa Mafifi unaendelea nao kwa kufanya kazi karibu na wananchi wa eneo hilo na kuhakikisha kuwa wananchi hawapati shida ya barabara katika kipindi hiki cha masika.

Hapo awali Akihutubia mamia ya wananchi walijitokeza katika hafla hiyo ya kukadhiwa cheti cha kuwa diwani wa kata hiyo Jully Sawani, MNEC Salim Asas alisema kuwa atatoa mifuko miambili ya saruji kwa ajili ya kutatua kero hiyo ya ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Kihesa na kuahidi kuwa ataitembelea shule hiyo kujua changamoto nyingine.

“Leo naanza kwa kutoa mifuko miambili ya saruji lakini nitakuja hapo shule kujionea changamoto nyingine za shule hiyo ili niweze kuzitatua kabisa na kuwaacha wananfunzi wakisoma kwa uhuru kwa lengo la kukuza kizazi chenye elimu bora na kuja kusaidia taifa katika kuleta maendeleo wote tunajua kuwa bila elimu huwezi kupata maendeleo hivyo nitasaidia sana kwenye elimu” alisema Asas
Asas aliwakata viongozi wa kata hiyo kuandaa bajeti ya kumalizia jingo hilo ambalo litaongeza ajira kwa wananchi wa kata hiyo ambao kwa sasa hali zao za kiuchumi zimedolola hivyoa atafanya linalowezekana kuhakikisha kuwa wananchi wa kata hiyo wanabadili na kuacha kuishi kimazoea.
“kata ya Kihesa anayoijua yeye ni ile yenye vijana wengi wasio na ajira ambao kwa bahati mbaya wamekuwa wakishughulishwa kwenye siasa badala ya kuhamasishwa kufanya shughuli za maendeleo” Alisema Asas

Hivyo MNEC  huyo ameshaanza kutekeleza ahadi zake kwa kuonye kuwa anaendana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ya hapa kazi tu na yeye ndio anafanya hivyo


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More