Wednesday, January 17, 2018

KADA WA CCM MICHAEL MLOWE AMPONGEZA MNEC SALIM ASAS KWA KUFANYA KAZI ZA KIMAENDELEO IRINGA

 Kada wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Michael Mlowe akiwa kwenye moja ya majukwa akikitumikia chama cha mapinduzi kueleza jinsi gani serikalia ya chama hicho inavyotekeleza wajibu wake kwa wananchi.
mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas akiwa jukwaani na diwani mpya wa kata ya Kihesa Jully Sawani.

Na Fredy Mgunda,Iringa

KADA wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Michael Mlowe amempongeza mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas kwa kazi anazizofanya za kuleta maendeleo katika mkoa wa huu.

Akizungumza na blog Mlowe alisema kuwa Asas amekuwa kiungo mkubwa kwa kuleta maendeleo hasa ukianga vitu alivyofinya hivi karibuni utajua kuwa jinsi gani amekuwa msaada kwa wananchi wa Iringa.

“Mimi naunga mkono juhudi za MNEC kwa kazi zake katika manispaa yetu ya Iringa hata mkoa mzi amekuwa akitatua changamoto nyingi ambazo hata serikali imeshindwa kuzitatua hivyo naomba wananchi waendelee kumuunga mkono kazi zake” alisema Mlowe

Mlowe alisema kuwa hivi karibu Asas alitoa ahadi kwa wananchi wa kata ya kihesa na akaanza mara moja kuitekeleza hivyo utagundua kuwa ni mtu wa maendeleo na anafaida kuwa kwa taifa leo

Ukiangalia utagundua kuwa mafundi wameanza kufanya shughuli za kimaendeleo za wananchi kama ilivyokuwa ahadi yake na ya MNEC Asas hivyo muda sio mrefu wananchi watapata ajira hapa

“Mwandishi ukiangalia hapa unawaona mafundi wanaendeleoa na kazi hivyo najua baada ya muda mufupi kila kitu kitakuwa kimemalizika na kuanza kutumika kwa faida ya wananchi wa kata ya kihesa” alisema Mlowe


Mlowe alisema kuwa anamshukuru MNEC Salim Asas kwa kutekeleza ahadi alizowahidi wakazi wa kihesa kwa kuwa tayari ameshatoa mifuko mia mbili (200) ya saruji katika shule ya sekondari ya Kihesa na tayari mafundi wapo kazini wameanza kumalizia ujenzi wa jengo la biashara ambalo litaongeza ajira kwa wakazi wa kata ya Kihesa na nje ya kata hii.


Aidha Mlowe aliwapongeza wanachama wa chama cha mapinduzi kwa kumchagua Salim Asas kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwani wamempata mtu sahihi katika kukikuza chama hicho manispaa ya iringa ambako ndio kuanaonekana kuna upinzani mkubwa.

“Saizi chama cha mapinduzi kimempata mtu sahihi kabisa wa kurudisha umoja wa wanachama na kuongeza wanachama wapya na kuuwa upizani kabisa kwa kuwa alisema kuwa yeye ni paka hivyo anaweza kufukuza panya wote waliopo manispaa ya Iringa” alisema Mlowe

Mlowe amewataka wanachama na wananchi wa mkoa wa Iringa kuendelea kuunga mkono mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas ili kuleta maendeleo na kuahakikisha Iringa inakuwa jiji kwa kuwa pasipokuwa na maendeleo ya kutosha Iringa hatuwezi kuwa jiji.


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More