
Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi ameishauri Serikali kuwapa vyeti au nakala ya vyeti vya kidato cha nne na sita watu ambao kwa namna moja au nyingine walipotelewa na vyeti hivyo.
Chumi alitoa ushauri huo kufuatia majibu ya Serikali kuwa imekuwa vigumu kuwapa vyeti watu waliomaliza masomo kabla ya mwaka 2009 kwa madai kuwa vyeti vya wakati huo havikuwa vinawekwa picha ya mhitimu.
Mbunge huyo alieleza kuwa, ili kuwaondolea usumbufu waliopoteza vyeti, serikali ikishathibitisha kuwa muhusika ndio mtu sahihi, basi apewe japo nakala ya cheti kama wanavyofanya Vyuo Vikuu.
Awali katika swali lake la msingi, Chumi alitaka kufahamu utaratibu unaotumika kwa mtu aliyepoteza cheti na kwanini kumekuwa na ucheleweshaji wa huduma hiyo kwa watu...