Sunday, April 30, 2017

STEVE LIHAWA: NIDHAMU YA WEUSI KUTAWALA KWENYE MICHEZO


Na Steve Lihawa, Ebony fm Iringa

Angalia hiyo Picha
Achana na ushindi na Joshua,
Achana na KO
Achana na rekodi zake joshua,achana na kila kitu kuhusu yeye,
Unamkumbuka martin Luther king,
I HAVE A DREAM?
unayemyona hapo ni mrusi kapiga magoti chini kwa mtu mweusi,mtu ambaye wazungu wanaamini watamtalawa daima,mtu asiye na akili,lakini eneo moja ambalo ngozi nyeusi haizuiliki ni kwenye kupambana,yes,huwa haiwezekani kumzuia mtu mweusi,unaanzaje?
Muangalie kante pale uingereza,muangalie serena William's, muangalie usain bolt,unaamzaje kumshinda mtu mweusi kwenye mapambano? Hapa ndipo wazungu wanapikubali rohoni lakini hawataki Usoni,nan kakwambia mrusi anaweza piga magoti kirahisi? Umeona wapi?
Ndio hii ndio maana halisi ya uwazi,wazungu wanapigwa nje lakini hawataki kusema,nikikumbuka nyakati zao wanatufanya wanavyotaka naumia,lakini dunia na maisha yanaendelea,sasa wazungu wanapiga magoti mbele ya ngzi nyeusi,dunia iktizama,
Maisha yana funzo sana,maisha yanazunguka Sana, malipo yako hapa hapa duniani,
Wazungu hawataki hii lakini hawawezi kuizuia,
Nenda kwenye music angalia ngozi nyeusi inavyotesa,Obama ametoka kuwaumiza jamaa juzi tu kuongoza Taifa kubwa akiwa na ngozi nyeusi,hawapendi lakini huwez zuia mafuriko,
Sitak ushindi wa Joshua lakini nimemuona mzungu akipiga magoti mbele ya ulimwengu,
......
Maisha yanazunguka popote ulipo usitumie nafasi yako na uwezo wako vibaya, huijui Kesho yako
😂😂😂😂
Huwa naandika sana hapa kuhusu waswahili hawa,hawaishi kunipa raha.. Babu zetu waliteseka sana gizani na ngozi zao gizani
Sasa sisi tunawatesa na ngozi zao kweupe

Saturday, April 29, 2017

AJALI USIKU HUU MAENEO IDARA YA MAJI MANISPAA YA IRINGA

Chanzo cha ajali hii ni mwendokasi wa Dereva uliopelekea kushindwa kupita vizuri kwenye mzunguko uliopo maeneo ya idala ya maji ndani ya Manispaa ya iringa lakini hakuna kifo bali kuna majeruhi tu Habari kamili itakujia hivi punde

MAJI MAPYA, MAJI MKWAWA KUINGIA SOKONI


SERIKALI imeipongeza familia ya mfanyabiashara Ahamed Huwel kwa kuitikia wito wa Rais John Magufuli wa kuifanya Tanzania nchi ya viwanda kwa kuanzisha kiwanda cha kisasa cha maji mjini Iringa yanayojulikana kwa jina la Maji Mkwawa.

Maji hayo yaliyoingizwa sokoni hivikaribuni yalizinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya magari Iringa yaliyodhaminiwa na kiwanda hicho, wiki iliyopita.

Akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa washindi wa shindano hilo la magari Mkuu wa Mkoa alisema; “Uzalendo ni pamoja na kujivunia kile tunachozalisha.”

Alisema Ahamed Huwel ametekeleza kwa vitendo kauli ya Rais Dk Magufuli ya Tanzania ya Viwanda kwa kuanzisha kiwanda hicho cha kisasa, kilichobaki ni kwa wadu kumuunga mkono.

“Kazi imebaki kwetu wana Iringa, ni muhimu tukamuunga mkono kwa kuwa wa kwanza kuyatumia maji haya,” alisema huku akiyapigia debe maji hayo kwa watanzania wengine.

Masenza alisema mbali na kiwanda hicho kuchangia pato la Taifa, kinatarajia pia kutoa ajira za moja kwa moja kiwandani na zile za mtu mmoja mmoja, kampuni au taasisi zitakazokuwa zikifanya biashara ya maji hayo.

Msimamizi wa Uzalishaji wa kiwanda hicho, Kevin Robert alisema kiwanda hicho ambacho mpaka sasa kimekwisha ajili wafanyakazi 23 wa kudumu kina uwezo wa kuzalisha lita 28,000 kwa saa.


“Na kitakuwa kifanya kazi kwa saa nane kila siku hivyo kuzalisha lita 224,000 kwa siku zitakazojazwa kwenye chupa za ujazo tofauti kwa kuzingatia mahitaji na kipato cha mtu,” alisema.

Alisema Maji Mkwawa yataingia sokoni wakati wowote kuanzia sasa baada ya kiwanda hicho kukamilisha taratibu chache za uzalishaji zilizasalia.

Akizungumzia tofauti ya maji hayo na ya viwanda vingine, Robert alisema; “Maji Mkwawa ni salama kwasababu yanatoka chini ya ardhi na yanazalishwa kwa kutumia tekenolojia ya kisasa.”

DK MSAMBATAVANGU AENDELEA KUSHIKILIWA NA POLISI

Tokeo la picha la jesca msambatavangu
Jeshi la Polisi Mkoani Iringa linaendelea kumshikilia Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa, Dk Jesca Msambatavangu anayetuhumiwa kumshambulia na kumsababishia maumivu makali mwilini mwanamke mmoja, ambaye jina lake bado halijafahamika.

Mpaka jana jioni wakili wake aliyetajwa kwa jina moja la Chaula na wadhamini wake walikuwa wakiendelea na taratibu za kumdhamini kada huyo wa CCM wa zamani huku kukiwa hakunataarifa zozote zinazoashiria kupewa dhamana hiyo.

Akizungumza kwa kifupi kuhusiana na tukio hilo juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi alisema kada huyo wa zamani wa CCM alikamatwa juzi mchana, akituhumiwa kutenda kosa hilo wiki iliyopita akiwa na wenzake ambao majina yao yamehifadhiwa kwakuwa wanaendelea kutafutwa.

RPC Mjengi alisema Msambatavangu na wenzake wanadaiwa kumshambulia mwanamke mmoja mkazi wa Kibwabwa (hakutajwa jina kwasababu za kiupelelezi) na kisha kumchoma sindano takoni ambayo mwanamke huyo hajui ni ya kitu gani.

Msambatavangu alikuwa miongoni mwa vigogo wa CCM ‘waliotumbuliwa’ hivi karibuni na kufukuzwa uanachama katika Mkutano Maalum wa CCM uliofanyika Machi, mwaka huu.

Baadhi ya marafiki na ndugu wa jirani wa Dk Msambatavangu jana walikusanyika nje ya ofisi ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa katika kile kilichoonekana kutaka kujua hatma ya mwanasiasa huyo ambaye pia ni mfanyabishara maarufu mjini Iringa.

Kabla ya kutoa amri iliyowataka watu hao kutawanyika katika eneo hilo kwa kile kilichoelezwa walikuwa katika mkusanyiko usio halali, Jeshi la Polisi liliwazuia watu hao kuingia ndani ya uzio wa ofisi hiyo ya RPC.

Baadhi ya waandishi wa habari waliofika katika ofisi hizo nao hawakupata fursa ya kuingia ndani ya uzio wa ofisi hizo ili kukutana na RPC kwa lengo la kupataa taarifa kamili ya kukamatwa kwa mwanasiasa huyo.

RIP MY GUARDIAN ANGEL ISABELLA






































I do not pretend to be older than many but the truth is that, I'm old enough to confess that life is indeed a mystery.

I've seen a Landlord becoming a tenant of his former tenant before his death. 

I know a student who became the Vice Chancellor in his former University with most of his lecturers still teaching under him.

I have seen a rejected person becoming the bread winner for a whole community. A victor becoming a victim. A driver conductor buying the bus of his master. And A borrower recruiting his erstwhile credit bank manager. 



In life, no one knows tomorrow & you can never trust life, because it is mysterious. 

Never ever forget. U may not know the full story, Don't be quick to judge. Every coin has two sides. 

Treat everyone during your life time fairly like your own & love and forgive as much as you live. 

So let us be humble, kind, love more & do not try to be smart in anything; for we do not know what tomorrow holds for us.

Five years ago, on 28th April 2012, my Guardian Angel Isabella Benita Bulengo was laid to eternal rest at Makongo Juu, Dar es Salaam at the Age of 5 years. RIP! My Guardian Angel Isabella.

Fr. James Byebazo Rugemalira Rutakwabyera


Friday, April 28, 2017

MIGODI INAYOMILIKIWA NA KAMPUNI YA ACACIA YAWA KIVUTIO KATIKA MAONESHO YA WIKI YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI.

Maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya mahala pa kazi yanayofanyika Moshi mkoani Kilimanjaro.
Maonesho haya yanayohusisha kampuni na Taasisi mbalimbali nchini yanaratibiwa na Wakala wa Usalama na Afya mahala pa Kazi (OSHA).
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,wakiweka sawa moja ya picha inayoonesha eneo ambalo shughuli za uchimbaji unafanyika.
Afisa Uhakiki na Usalama katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA,Amina Mohamed akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,wakitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda hilo katika maeonesho ya wiki ya usalama mahala pa kazi ndani ya viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi.
Afisa Afya katika Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu ,Tumaini Sylivanus akitoa maelezo ya namna wanavyotoa huduma ya Afya kwa wafanyakazi wa Mgodi huo pindi wapatapo matatizo.
Mmoja wa Wakazi wa Kilimanjaro akipewa maelekezo ya namna ya kutumia kifaa maalumu kinachotumika katika zoezi la uzimaji wa moto pindi yatokeapo majanga ya Moto.Nyuma yake ni mmoja wa wafanyakazi wa Mgodi wa Bulyanhulu unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA.
Afisa Viwango wa Mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu,Setieli Kimaro akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliotembelea banda la modi huo unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA.
Afisa Usalama katika Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,Deogratius Nyantabano akitoa maelezo kwa wanafunzi waliotembelea banda la mgodi huo katika maonesho ya wiki ya usalama na afya mahala pa kazi yanyofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi ,Kilimanjaro.
Afisa Usalama katika Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,Mustapher Mlewa akieleza jambo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea Banda hilo.
Daktari kutoka Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni ya ACACIA,Dkt Ludovick Silima akitoa maelezo juu ya usalama kwa mmoja wa wananchi waliofika katika banda la mgodi huo wakati wa maonesho ya wiki ya usalama na afya mahala pa kazi yanayoendelea katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
Afisa Mazingira katika Mgodi wa north Mara ,Sara Cyprian akionesha picha na maelezo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Mgodi huo katika maonesho ya wiki ya usalama na afya mahala pa kazi.
Afisa Usalama katika mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya ACACIA,Samweli Nansika (aliyenyoosha kidole) akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la mgodi huo.
Mkuu wa Idara ya Usalama na uokoaji katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara ,Emanuel Erasto(katikati) akitoa maelezo namna amavyo wanaweza kumuokoa mtu aliyepata athari iliytokana na kemikali.
Eneo maalumu la kumuogesha mtu aliyepata athari ya kemikali.
Afisa usalama akita huduma ya kumsafisha mtu aliyepata athali ya kemikali akiwa nje ya bafu hilo la kumuogeshea ili na yeye asipate madhara.
Wafanyakazi wa Mgodi wa Buzwagi wakionesha namna ambavyo wanaweza msaidia mtu aliyepatwa na janga la Moto.
Kifaa Maalumu kinachotumika katika kubeba mwili wa mtu aliyepata madhara akiwa katika shimo wakati wa uchimbaji wa Dhahabu.
Mmoja wa wafanyakazi wa Mgodi wa Bulyanhulu akitoa maelezo kwa wananchi walitembelea banda hilo namna ambavyo wanaweza kunyanyua Gari pamoja na Mawe yaliyomuangukia mtu wakati akitekeleza majukumu yake kwa kutumia kifaa maalumu kinachojazwa upepo (Air Bag).
Mkuu wa Idara ya Usalama na Uokoaji katika Mgodi wa North Mara ,Emanuel Erasto akitoa maelezo namna wanavyoweza kumukoa mtu aliyepatwa madhara akiwa chini ya mgodi .
Dkt Ludovick Silima akitoa ufafanuzi kwa wananchi waliotembelea banda la Mgodi wa Buzwagi.
Afisa Mahusiano katika Mgodi wa Bulyanhulu akitoa maelezo ya namna Mgodi huo unavyo tekeleza majukumu yake ukitoa kipaumbele katika masuala ya Usalama na Afya kwa watumishi wake.
Afisa Uhusiano wa Mgodi wa Buzwagi ,Magesa Magesa akitoa maelezo namna mgodi huo ulivyoshiriki katika shughuli za maendeleo ikiwemo ujengaji wa vyumba vya madarasa,zahanati,maji pamoja na suala la kuhamasisha michezo katika maeneo yanayozunguka mgodi huo.

Na Dixon Buagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More