Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Deus Sangu, akiwasilisha hotuba yake mbele ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkoa wa Geita, Menejimenti ya Mgodi wa Geita na watendaji wa Ofisi yake katika ziara ya kufuatilia utekelezaji wa Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi na Sheria nyingine za kazi katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Deus Sangu, akiwasilisha hotuba yake mbele ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Mkoa wa Geita, Menejimenti ya Mgodi wa Geita na watendaji wa Ofisi yake katika ziara ya kufuatilia utekelezaji wa Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi na Sheria nyingine za kazi katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML).
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Geita, Menejimenti ya Mgodi wa Geita na watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Deus Sangu katika ziara ya kufuatilia utekelezaji wa Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi na Sheria nyingine za kazi katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Deus Sangu, akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML), Bw. Ashraf Suryaningrat, mara baada ya kuhitimisha ziara ya kufuatilia utekelezaji wa Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi na Sheria nyingine za kazi katika Mgodi huo.Na Fredy Mgunda,Geita
Wito umetolewa kwa
makampuni makubwa ya uchimbaji madini nchini kuwekeza katikakuwawezesha
wachimbaji wadogo katika nyanja mbalimbali ikiwemo teknolojia za kisasa na
usimikaji wa mifumo ya usalama na afya mahali pa kazi ili kujenga
uchumijumuishi unaotokana na sekta ya madini.
Wito huo umetolewa na serikali kupitia Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Deus Sangu, alipofanya
ziara ya kufuatilia utekelezaji wa Sheria yaUsalama na Afya Mahali pa Kazi na
Sheria nyingine za kazi katika Mgodi wa Dhahabuwa Geita (GGML).
Waziri Sangu ameipongeza menejimenti ya Mgodi huo
kwa kuzalisha ajira nyingi kwaWatanzania ambapo GGML imeajiri jumla ya
wafanyakazi 2,366 moja kwa moja na4,629 wameajiriwa kupitia wakandarasi
mbalimbali wanatoa huduma katika Mgodi waGGML.
Sambamba na pongezi hizo, Waziri mwenye dhamana ya
masuala ya kazi ameutakaMgodi huo kuhakikisha kwamba shughuli zake zinakuwa na
athari chanya katikauchumi wa jamii zinazowazunguka kwa kutoa fursa za kazi za
muda mfupi ikiwemokuwezesha miradi mbalimbali ya kijamii.
Aidha, Waziri Sangu ameipongeza GGML kwa kuchagua
suala la usalama na afya kwawafanyakazi kuwa tunu yao ya kwanza katika shughuli
zao za uchimbaji na uchakatajiwa madini jambo ambalo limewafanya kujenga mifumo
madhubuti ya kulinda afya nausalama wa wafanyakazi inayozingatia matumizi ya
teknolojia za kisasa.
“Ninawapongeza kwa kuweka usalama na afya kama
tunu yenu ya kwanza na hiiimejidhirisha katika wasilisho lenu mlilofanya hapa
ambapo masuala ya usalama naafya yamechukua nafasi ya juu zaidi ya biashara
mnayofanya,” ameeleza Waziri Sangu na kuongeza:
“Pongezi hizi inastahili pia Taasisi ya OSHA
ambayo imekuwa ikiwaongoza katikakutekeleza hayo kupitia usimamizi mzuri wa
Sheria Na.5 ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 na miongozo
mbalimbali chini ya sheria hiyo ambayowamekuwa wakiitoa kupitia kaguzi zao za
mara kwa mara.”
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa katika ziara
hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Geita,Hashim Abdallah Komba, amesema OSHA ni miongoni
mwa Taasisi zenye msaadamkubwa katika kuwezesha shughuli mbalimbali za kiuchumi
kufanyika kwa tija katikaMkoa wa Geita.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi. Khadija
Mwenda, amesema ziara hiyo, inalenga kuona jinsi OSHA inavyoshirikiana na wadau
wake kutekeleza Sheria yaUsalama na Afya mahali pa kazi ambayo dhima yake kuu
ni kulinda nguvukazi ya Taifa dhidi ya ajali na magonjwa yatokanayo na kazi pamoja
na kulinda uwekezaji kupitiakuzuia uharibifu wa mali.
Awali, menejimenti ya GGML iliwasilisha taarifa
juu ya shughuli zao iliyoainisha jinsiafya na usalama wa wafanyakazi
unavyozingatiwa katika shughuli husika. Miongonimwa masuala yaliyoelezwa katika
taarifa hiyo ni pamoja na historia ya mgodi ambapoimeelezwa kuwa madini katika
mgodi huo yaligunduliwa mnamo mwaka 1898 nauchimbaji rasmi kuanza mwaka 1999.






Monday, February 23, 2026
mwangaza wa hbari







0 comments:
Post a Comment