Friday, September 8, 2017

MBUNGE COSATO CHUMI AMALIZA ZIARA YAKE NCHI KOREA KWA MAFANIKIO MAKUBWA

 Mbunge wa jimbo la halmashauri ya Mji wa Mafinga Cosato Chumi akiwa na askari polisi alipotembelea eneo linalotenganisha mipaka ya Korea kusini na Korea kaskazini
 Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa eneo hilo la mpakani.
Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Cosato Chumi amaliza ziara yake ya kimkakati kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo hili.

Akizungumza na blog hii Chumi alisema kuwa amefanikiwa kukutana na viongozi wa mashirika mbalimbali ya watu binafsi na serikali lengo likiwa kutafuta fursa kwa ajili ya wananchi wa jimbo la Mafinga Mjini.

"Katika siku yangu ya mwisho pamoja na kutembelea eneo linalotenganisha Korea Kusini na Korea Kaskazini, nimekutana pia na watendaji wa NGO ya Kimataifa ya Korea ya Good Neighbor, tumejadili mambo mengi, kubwa ikiwa ni ushirikiano kati yao na halmashauri ya Mji wa Mafinga katika sekta za maji, Elimu na Afya" alisema Chumi

Aidha Chumi alisema taasisi nyingi zimelipokea andiko lao kwa ajili ya ushirikiano baina ya taasisi hivyo na viongozi wa halmashauri ya mji wa Mafinga.

"Wamepokea andiko letu linalojieleza kwa kina, na Mungu akibariki watatuweka katika mipango yao ya mwakani"

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More