Monday, September 18, 2017

JET yapaza sauti, Yaitaka Serikali kuingilia kati mgogoro wa Ardhi Kilwa

Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira nchini (JET) kimeitaka serikali kuingilia kati mgogoro wa ardhi uliopo baina ya wanavijiji wa Mavuji, Migeregere, Liwiti na Nainokwe wilayani Kilwa na Kampuni ya Uwekezaji ya Bioshape Ltd ,uliobuka baada ya kampuni hiyo kuitelekeza ardhi ya vijiji hivyo kwa muda mrefu. Akizungumza na wanahabari mapema jana Septemba 17, 2017 jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Bodi ya JET, Leah Mushi amesema muwekezaji huyo amekiuka makubaliano ya umiliki wa ardhi takribani hekta 64,000 ikiwemo kwa kutotimiza malengo ya mradi sambamba na kutotekeleza ahadi aliyoahidi ya kuboresha huduma za jamii kwenye vijiji husika. Kufuatia ukiukwaji huo uliofanywa na kampuni hiyo, Mushi ameitaka serikali kuchukua hatua kwa kuwarudishia wanavijiji hao ardhi yao ili wajikwamue kiuchumi, kama ilivyofanya kwa wawekezaji wengine wasioendeleza ardhi zao “Kutokana na ongezeko la watu na shughuli za kiuchumi, serikali haina budi kuwarudishia ardhi hiyo ili serikali za vijiji ziweze kumiliki misitu na rasilimali nyingine zitakazowawezesha kujikwamua kiuchumi bila kutegemea ruzuku kutoka halmashauri ya wilaya,” amesema. Kwa upande wake Aisia Rweyemamu miongoni mwa waandishi wa habari za mazingira aliyefanya utafiti wa uwekezaji wa kilimo cha mibono, amesema kufuatia uchunguzi walioufanya hasa kwenye vijiji hivyo vinne walibaini kuwa uwekezaji huo uliathiri wananchi baada ya muwekezaji huyo kusitisha miradi huku akihodhi ardhi kubwa ambayo wananchi hawawezi kuitumia. Hata hivyo, Rweyemamu amesema Kampuni ya Bioshape Ltd baada ya kushindwa kuendeleza ardhi hiyo kwa zaidi ya miaka mitano, walitaka kuhamisha uwekezaji huo kwa kampuni nyingine ya uwekezaji kitendo kilichopingwa na wananchi wa vijiji hivyo. Naye Mosses Masenga alibainisha kuwa, kufuatia uchunguzi walioufanya kwenye vijiji hivyo waligundua kwamba muwekezaji alivyochukua eneo hilo alifoji hati ya tathimini ya athari za kimazingira, pamoja na kumilikishwa eneo hilo kinyume na sheria ikiwemo kuongezewa muda wa kumiliki ardhi hiyo kutoka miaka 33 hadi zaidi ya 90.
Mmiongoni mwa Waandishi wa Habari za Mazingira aliyefanya Utafiti wa kina juu y a tukio hilo, Bi. Aisia Rweyemamu akizungumza katika mkutano huo wa waandishi wa Habari mapema jana Septemba 17,2017, Jijini Dar es Salaam. Anayemfuatia ni Mjumbe wa Bodi ya Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET), Bi. Leah Mushi na mwishi ni Bw. Moses Masenga, mwanahabari wa Mazingira.
Mmiongoni mwa Waandishi wa Habari za Mazingira aliyefanya Utafiti wa kina juu y a tukio hilo, Jimmy Charles akizungumza katika mkutano huo wa waandishi wa Habari mapema jana Septemba 17,2017, Jijini Dar es Salaam. Anayemfuatia ni Mjumbe wa Bodi ya Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET), Bi. Leah Mushi na mwishi ni Bw. Moses Masenga, mwanahabari wa Mazingira.
Mwanahabari wa Mazingira, Moses Masenga akifafanua juu ya tukio hilo kwa waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa JET ilipota ripoti juu ya hali ya mgogoro wa Ardhi Kilwa. Wengine ni Mjumbe wa Bodi ya JET, Bi. Leah Mushi akifuatiwa na Mwanahabari, Bi. Aisia Rweyimamu
Mjumbe wa Bodi ya JET, Bi. Leah Mushi akisoma ripoti maalum kwa vyombo vya Habari wakati wa mkutano huo wa kuelezea mgogoro wa Ardhi baina ya mwekezaji na wanakijiji Kilwa, Pwani. Kulia ni Mwanahabari wa Mazingira Moses Masenga na kushoto ni Bi. Aisia Rweyimamu ambao waliweza kufanya utafiti wa kihabari juu ya matukio hayo.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More