Friday, September 29, 2017

JAFO: WATENDAJI MSILETE LELEMAMA USIMAMIZI MIRADI YA MAENDELEO

 Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akisisitiza jambo alipokuwa akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua Kituo cha Afya Kintinku wilayani Manyoni, Wengine ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu na Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki (CCM) Mhe Daniel Mtuka  Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakikagua chumba cha kuhifadhia maiti katika kituo cha Afya Kintinku wilayani Manyoni. Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akitembelea na kukagua mradi wa maji Kintinku/Lusilile wilayani Manyoni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Manyoni...

MAMIA WAFUNGULIWA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA INJILI JIJINI MWANZA

 Na George Binagi-GB Pazzo Wakazi wa Jiji la Mwanza wakiwemo waumini wa dini mbalimbali wameendelea kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano mkubwa wa injili ulioandaliwa na kanisa la kanisa EAGT Lumala Mpya chini ya Mchungaji Dkt.Daniel Moses Kukola. Jana mamia ya wananchi walijitokeza kwenye mkutano huo unaofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza na kukutana na mlipuko mkubwa wa injili kutoka kwa watumishi wa Mungu akiwemo mwinjilisti Rojas Matias kutoka Marekani chini ya huduma ya MORE International Ministry. Aidha waimbaji Ambwene Mwasongwe, Mbilikimo Watatu, Samwel Lusekelo, Joseph Rwiza, Sam D, Havillah Gospel Singers na wengine wengi wameendelea kukonga nyoyo za wahudhuriaji kwenye mkutano huo. “Maandalizi ya...

WATANZANIA WANG'ARA SHINDANO LA MWANDISHI BORA WA SAYANSI NA KILIMO AFRIKA

 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona (kushoto), akimkabidhi cheti Mwandishi wa Star Tv Dino Mgunda kuwa mshindi wa pili kwa waandishi wa Televisheni kwenye shindano hilo lililofanyika jana nchini Uganda.  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona, akimkabidhi cheti Mwandishi wa Tanzania Koleta Makulwa kutoka Radio Free Afrika ambaye alipata tuzo na kuwashinda wenzake ambao walikuwa wanashindana katika eneo la Radio.  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona, akimkabidhi cheti Mwandishi wa Tanzania wa gazeti la Guardian,...

HATIMAYE WANANCHI WANAOTAKIWA KUPISHA MRADI WA SHANTA GOLD MINE WILAYANI IKUNGI WATEKELEZEWA MALIPO YAO

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliowahusisha wananchi wa Kijiji cha Mang’onyi, Sambaru na Mulumbi kwa ajili ya kulipa fidia za wanufaika kwa ajili ya kupisha Mradi wa Kampuni ya uchimbaji madini ya Shanta Gold Mining Ltd. Wananchi wa Kijiji cha Mang’onyi, Sambaru na Mulumbi wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Mhe Miraji Jumanne Mtaturu Akizungumza katika mkutano wa hadhara kwa ajili ya kulipwa fidia za wanufaika kwa ajili ya kupisha Mradi wa Kampuni ya uchimbaji madini ya Shanta Gold Mining Ltd. Meneja wa Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Shanta Gold Mining Ltd Philbert Rweyemamu akielezea utaratibu wa ulipaji fidia kwa wanufaika. Wananchi...

SEKTA YA MANUNUZI YA MTANDAONI NA CHANGAMOTO ZAKE NCHINI TANZANIA

Na Jumia Travel Tanzania Miongoni mwa sekta ambazo zimewapatia utajiri mkubwa wafanyabiashara mbalimbali duniani ni pamoja na biashara kwa njia ya mtandao. Leo hii ukiyataja majina ya kampuni kama vile Alibaba au Amazon ni watu wachache wasioyafahamu licha ya kutokuwepo nchini Tanzania. Waasisi wa makampuni hayo wamo kwenye orodha ya watu matajiri duniani, Bw. Jeff Bezos mwasisi wa Amazon ni tajiri nambari 3 huku Jack Ma ambaye ni mwasisi wa Alibaba yeye ni tajiri nambari 23. Utajiri wa wafanyabiashara hawa sio kama wanamiliki biashara katika nchi mbalimbali bali uwezo wa makampuni yao kuwafikia wateja mahali popote walipo. Kuwafikia wateja hao Jumia Travel ingependa kukufahamisha si kwa njia nyingine bali ni kupitia mtandao wa...

DAWA NI KULALAMIKA AU KUCHUKUA HATUA?

Na Emmanuel J. Shilatu  Mara nyingi Rais Magufuli amekuwa akitoa kauli akisisitiza Watu kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili wajiimarishie kipato binafsi. Watu wanapolalamika kuwa maisha ni magumu, hakuna pesa mitaani jibu analolitoa Rais Magufuli anasisitiza Watu kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kupambana na hali ya maisha iliyopo. Rais Magufuli sio kiongozi wa kwanza nchini kusisitiza juu ya Wananchi kufanya kazi kwa bidii. Kumbukumbu zinaonyesha hata Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere naye pia alikuwa akisisitiza juu ya Watu kufanya kazi kwa bidii. Wakati tunapata uhuru wetu mwaka 1961 kutoka kwa Waingereza kila Mtanganyika alikuwa na maana yake kichwani ya kuelewa nini maana ya uhuru....

Page 1 of 69412345Next
Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More