Friday, August 25, 2017

MBUNGE GRACE TENDEGA KUWASAIDIA VIJANA KUPATA MIKOPO YENYE MASHARTI NAFUU

 Mbunge wa viti maalumu kutoka chadema Grace Tendega akipokea risala kutoka kwa Obed Mazika wakati alipokwenda kupokea kero zinazowakabili wanachi wa ifunda ili kuweza kuzipeleka bungeni


NA RAYMOND MINJA IRINGA 

Vijana wanaojishungulisha na shughuli za uendeshaji boda boda na upigaji debe katika stendi ya Ifundi kwenye kijiji cha Ifunda  kata ya ifunda wameiomba halimashauri ya wilaya ya Iringa kuweza kuwapatia mikopo inayotokana tengo la asilimia tano kwa ajili ya vijana ili kuweza kujikwamua kiuchumi .

Vijana hao walisema kuwa licha ya kujiunga katika vikundi vidogo vidogo vya ujasiriliamali lakini hawajawahi kubahatika kupata mikopo kwani mikopo hiyo imekuwa ikitolewa kirasimu kwa kile wanachodai ni itikadi za kisiasa .

Akizungumza mbele ya mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha demkorasia na maendeleo Chadema Grace Tendega aliyeenda kupokea kero zinazaowakabili wananchi hao moja ya Vijana anayeendesha bodaboda Ayubu kiwelo  alimuomba mbunge huyo kuwasaidi kupeleka kilio chao kwenye halmashauri ili nao waweze kunufaika na tengo la asilimia tano kwa ajili ya  vijana .

Kilwelo  alisema kuwa katika kipindi cha kampeni waliahidiwa ahadi lukuki ikiwemo kujiunga katika vikundi ili waweze kupatiwa mikopo ya kujiendeleza kwenye biashara ndogo ndogo lakini mpaka leo hii hakuna hata kikundi kimoja kilichopata mikopo hiyo .

“Mhh toka chaguzi umekwisha hakuna mbunge wa viti maalumu au mbunge wa kuchaguliwa ambaye alishawahi kuja hapa kutusikiliza kero zetu tunazo kero nyongi ikiwemo swala la maji lakini hili la mikopo kwa vijana ndio linazidi kutumiza tunasikia wenzetu wanapata lakini sisi hatupati na hii nikutokana na kusema eti tulichagua upinzani hebu katusaidie maana sisi sote ni watanzania ”

Akijibu ombi hilo Grace Tendega aliwataka vijana hao kuwa wavumilivu ili kuweza kufuatilia na kujua ni kwanini vijana hao hawapatiwi mikopo ili hali kuna asilimia tano zilizotegwa kwa ajili ya vijana bila ya kuangalia itikadi za kisiasa .

Tendega alisema ni haki kwa vijana hao kupata mikopo hiyo inayopatikana kwa riba nafuu kwani fedha hizo zinatokana na kodi inayokatwa katika bidhaa mbambila wanazo tumia katika matumizi yao ya kila siku

“Hii mikopo sio takrima ni haki yenu kupata na pindi pia munapopata fedha hizo sio kwa ajili ya kula au kuongeza mke wa pili bali munatakiwa kuzizungusha na kupata faidi na kurudisha kile mlichokopa ili na wengine waweze kukopeshwa hivyo niwaahidi kesho kuna baraza nitazungumza nao ili nijue tatizo ni nini mpaka nyie mukose mikopo  hiyo ila niwasihi  kuweni wavumilivu alisema” Tendega 

Awali akisoma risala inayohusu kero ya maji katika kijiji hicho  kwa niaba ya wanachi wa kijiji hicho Obed Mazika alisema  kuwa wamekuwa wakipata adha kubwa ya maji safi na salama  kwani wamekuwa wakinunua ndoo moja ya maji kwa shilingi mia tano jambo linalowafanya kuendelea kuwa na maisha duni


Alisema kuwa mradi shirikishi wa kufufua miundombinu  kwa kushirikiana na wanachi na mkandarasi atakayepewa tenda hiyo tayari wameshaanza mchakato wa kuchangishana fedha na inahitajika kiasi cha shilingi miloni tano inayotakiwa kusoma katika akauntu ya kijiji hicho ili iweze kusaidia katika mchakato huo 

Akijibu hutuba hiyo Tendege aliahidi kuwasaidia wanakijiji hao kwa kushirikiana nao bega kwa bega ili kuweza kutatua kero ya maji inayokabili inayowakabili na kuahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni mbili kwa ajili ya kusaidia  kufufua miundombinu ya maji katika kijiji hicho

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More