Saturday, August 26, 2017

DC MTATURU WAZAZI HAKIKISHENI WANAFUZI WANAPATA CHAKULA CHA MCHANA SHULENI

 Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mkoani singida Miraji Mtaturu akikagua chakula kilichopo na ubora wake katika shule ya sekondari ya Makiungu kwa dhamira ya kuboresha upatikanaji wa elimu bora kwa wanafunzi wa Wilaya hiyo

Na fredy Mgunda, Ikungi Singida

Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoani singida Miraji Mtaturu amezipongeza shule zote zinazotoa huduma ya chakula cha mchana kwa  wanafunzi ili kuboresha elimu kwa wananchi wa wilaya hiyo kwa manufaa ya taifa.

Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea shule ya sekondari ya makiungu  Mtaturu alisema kuwa amefurahishwa na mradi wa kutoa chakula cha mchana kwa walimu na wanafunzi wa baadhi ya shule zilizopo wilayani humu.

"Sio wazazi wote wanauwezo wa kuwapa watoto wao chakula cha mchana hivyo imekuwa kero sana katika Juhudi za kukuza elimu kwa wanafunzi ambao familia zao ni duni hivyo mpango huu wa wanafunzi na walimu kupata chakula cha mchana shuleni kinaongeza maalifa kwa walimu na wanafunzi "alisema Mtaturu

Aidha Mtaturu aliwataka wananchi na wazazi kuziunga mkono shule zote zinazotoa huduma ya chakula cha mchana kwa watoto wao kwa sababu ukifanya hivyo utaifanya elimu ya wanafunzi wenu kukuwa kutokana na mahitaji wanayoyapata shuleni.

"Unajua hakuna kitu kibaya kama njaa,ukiwa na njaa huwezi kufanya shughuli yoyote ile na utakuwa na ongezeko la msogo wa mawazo kitu kitakachosababisha kutoka kwenye mstari ulikuwa umepanga kuupitia ili upate mafanikio" alisema Mtaturu
Lakini Mtaturu alisisitiza walimu kufundisha kwa weledi walipowe wakiwa nao wanafunzi hivyo ni lazima mwalimu uwafundishe wanafunzi kwa ustadi wa hali ya juu ili hata wewe mwalimu ujipime uwezo wako katika fani hiyo ya ualimu.

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekonadari ya Makiungu walimpongeza mkuu wa wilaya kwa kuamua kuweka mpango huo wa chakula cha mchana kwani utawasaidia kupata muda mwingi wa kujisomea na kusoma kwa pamoja na hapo ndio tutakuza maarifa katika vichwa vyetu.

"Yaani tukitoka shule tukirudi nyumbani tulikuwa tunaanza upya kujipikia kutokana na uwezo wa familia zetu kwani kufanya hivyo kunasababisha kusahau nini ulifundishwa na kuanzia kuwaza kupika kwa kuwa njaa inakuwa inatukabili"walisena baadhi ya wanafunzi

Kwa upande wao walimu wa shule ya sekondari ya Makiungu aliwaomba wazazi kuwachangia kwenye huduma hii ya kutoa chakula cha mchana kwa kuwa kinagharama kubwa na uendeshaji wake mgumu pia hivyo tu naomba mziunge mkono shule zote zinazotoa huduma ya chakula cha mchana.

"Kila siku bei ya vyakula inapanda na kushuka hivyo unaweza kukuta takribani miezi sita hadi saba chakula kinapanda bei hivyo inawaletea ugumu kutoa huduma ya chakula bora kwa wanafunzi hivyo tunaomba wazazi na wananchi wote kuziunga mkono juhudi za shule zinazotoa huduma ya chakula cha mchana" walisema walimi.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More