Wednesday, August 16, 2017

MAKAMU MWENYEKITI BAVICHA TAIFA PATRICK OLE SOSOPI KUANZA ZIARA KATIKA JIMBO LA ISIMANI


Makamu Mwenyekiti Baraza la Vijana wa CHADEMA  Taifa,  Mh.  Patrick Ole Sosopi,  Jana tarehe 15.08.2017 Alifanya ziara Jimbo la ISIMANI Na kugawa BAISKELI  kumi (10)  kwa Walemavu wa Miguu  na Wanaotambaa (People with Disability)

Kata za zilozonufaika ni

1. Mahuninga, kijiji Makifu
2. Idodi, kijiji cha Idodi
3. Mlowa, Kijiji cha Malizamga
4. Itunundu, kijiji cha Idunundu
5. Mboliboli, kijiji cha Mbugani
6. Migoli, Wanufaika  ni 2 kijiji cha Migoli
7. Nyang'oro, kijiji cha cha Chamndindi
8. Kihorogota, kijiji cha Isimani
9. Kising'a, Kijiji cha Ilambilole

Mh. Patrick Ole Sosopi aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo La Isimani kupitia CHADEMA,  alitafuta Msaada huo kutoka shirika la Kimarekani Kupitia Kanisa la kiinjili la Kilutherani,  Dayosisi Ya Iringa.

Hii ilikuwa  ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi alizoahidi kwa makundi mbalimbali wakiwemo walemavu wakati wa kampeni Jimbo la ISIMANI 2015.

Ole Sosopi aliomba Msaada huo tangu September 2016 kukiwa kuna uhitaji wa watu 87 Katika jimbo La Isimani

Ugawaji wa Baiskeli hizi ulifanyika jana Tarehe  15.08.2017, Jimbo La Isimani, Kata ya Migoli

Ole Sosopi alieleza kwamba pamoja na uundwaji wa Baiskeli zote (Assembling)
Pia aligharamia Kuwasafirisha Watu Wenye Ulemavu Kutoka sehemu Mbalimbali Za Jimbo Mpaka Migoli pamoja na kupata Chakula Na Malazi.

Sanjari na hayo Ole Sosopi amewashukuru na kuwaomba  kuendelea kuwasaidia kwani uhitaji bado  ni mkubwa na yeye kama kiongozi aliwasisitiza na kuwaomba kuendelea kuwasaidia waliobaki kwani uhitaji ni mkubwa

Pia Ole Sosopi amewaomba wale wote waliopata Msaada huo kuzitunza Baiskeli hizo kwani sasa zitawasaidia kwenye shughuli zao za kimaendeleo na kiuchumi kwani zinauwezo wa kubeba bidhaa ndogo ndogo,  lakini pia baiskeli hizo zinaweza kusaidia kuchota Maji ikiwa kuna ukosefu wa maji katika maeneo mengi  ya Isimani na kusisitiza kuwa Baiskeli hizo ni  Rafiki kwa Mazingira ya Vijijini.

Ole Sosopi, kipekee Amewashukuru sana Ndg. B Mkocha Na Mkewe Bi. Maria Kwa Moyo wao wa dhati wa kukubali ombi la kumsaidia kupata baiskeli hizo na kuamua kuisaidia jamii zenye mahitaji maalum Kwa jimbo la Isimani,   amewashukuru pia kwa nia yao ya kukubali kuendelea kusaidia  misaada mbalimbali kwa jamii ya Watu wa Isimani nje ya msaada huu.

Mwisho Ole Sosopi aliwashukuru wadau wote walio saidia kufanikisha zoezi zima.

©Jackson Mnyawami,
Katibu BAVICHA Mkoa wa Iringa.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More