Sunday, July 30, 2017

MCHAPALO WA MIAKA 50 YA BENKI YA NBC WAFANA JIJINI MWANZA

Na George Binagi-GB Pazzo Jana Julai 28,2017 usiku wa kuamkia leo jumamosi, mchapalo (sherehe) wa kusherehekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwa benki inayolitumikia Taifa la Wachapakazi, NBC umefana Jijini Mwanza ambapo benki hiyo imekutana na wadau wake wakiwemo wafanyabiashara. Kaimu Mkurugenzi wa benki ya NBC, Theobald Sabi alisema maadhimisho hayo yamefanyika Jijini Mwanza ikizingatiwa kwamba Jiji hilo ni la pili kwa ukubwa nchini na kwamba inao wateja wa muda mrefu wanaohudumiwa kwenye matawi yake matatu hivyo ni jambo jema kujumuika nao pamoja. "Hakika NBC ina historia ndefu katika kujenga uchumi wa nchini yetu, ni jambo lisilopingika kwamba NBC ni mama wa benki za kibiashara hapa Tanzania". Alidokeza Sabi huku akiwashukuru wafanyakazi wa benki hiyo waliojawa uzalendo, umakini na ubunifu katika kazi. Mkurugenzi wa Bodi ya NBC, Dr.Kassim Hussein alisema moja ya hatua za benki hiyo ni kuwa kitovu cha malipo yote nchini (National Payment System) mfumo ambao hadi sasa unategemewa nchini. Alidokeza kwamba miaka ya 70 mbali ya kutoa huduma nchini nzima, vile vile benki hiyo ilikuwa ikitoa huduma kwa njia ya mawakala, ikawa mwanzishi wa mobile banking pamoja na huduma za bima. Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Merry Tesha aliipongeza benki ya NBC kutokana na mapinduzi yake kwenye sekta ya kifedha nchini na kuiomba kuwekeza moja kwa moja ama kwa ubia katika utekelezaji wa azima ya serikali ya ujenzi wa viwanda nchini ikiwemo kutoa mikopo kwa wawekezaji wa ndani. [caption id="attachment_27640" align="alignnone" width="620"] Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Merry Tesha akizungumza kwenye mchapalo huo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.[/caption] [caption id="attachment_27641" align="alignnone" width="620"] Kaimu Mkurugenzi wa benki ya NBC nchini, Theobald Sabi, akizungumza kwenye mchapalo huo wa miaka 50 ya NBC[/caption] [caption id="attachment_27642" align="alignnone" width="620"] Mkurugenzi wa bodi ya benki ya NBC, Dr.Kassim Hussein, akizungumza kwenye mchapalo huo[/caption] [caption id="attachment_27643" align="alignnone" width="620"] Mmoja wa wateja wa benki ya NBC akitoa salamu za shukurani kwa niaba ya wateja wengine kwenye mchapalo huo[/caption] [caption id="attachment_27644" align="alignnone" width="620"] Burudani kutoka kikundi cha ngoma asili, Mwanza Dance Group kikitumbuiza[/caption] [caption id="attachment_27645" align="alignnone" width="620"] Mgeni rasmi, viongozi wa NBC na wageni waalikwa wakifungua muziki kwenye mchapalo huo[/caption] [caption id="attachment_27646" align="alignnone" width="620"] Afisa Mahusiano Jiji la Mwanza, Elirehema Kaaya (kushoto), akimpongeza Mkurugenzi wa Bodi ya NBC, Dr.Kassim Hussein (kulia) kwa utendaji kazi mzuri wa benki ya NBC nchini.[/caption] [caption id="attachment_27647" align="alignnone" width="620"] Mkurugenzi wa Bodi ya NBC, Dr.Kassim Hussein (kulia), akipokea pongezi kutoka kwa Afisa Mahusiano Jiji la Mwanza, Elirehema Kaaya kuhusu miaka 50 ya benki ya NBC kulitumikia Taifa la Wachapakazi.[/caption] [caption id="attachment_27648" align="alignnone" width="620"] Mchapalo/ sherehe za miaka 50 tangu kuanzishwa benki ya NBC[/caption] [caption id="attachment_27649" align="alignnone" width="620"] Mgeni rasmi, viongozi wa NBC pamoja na wageni waalikwa kwenye picha ya pamoja[/caption] [caption id="attachment_27650" align="alignnone" width="620"] Selfie kufurahia miaka 50 ya benki ya NBC[/caption] [caption id="attachment_27651" align="alignnone" width="620"] Hakika Ukubwa Dawa, BMG tunatoa pongezi za dhati kwa benki ya NBC kwa kutimiza miaka 50 tangu kuanza kulitumikia Taifa la Wachapakazi Tanzania.[/caption]
Tazama HAPA uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki ya NBC Jijini Mwanza

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More