Tuesday, July 18, 2017

DIWANI LEAH MLELEU AVIFIKIA VIKUNDI VYA AKINA MAMA WA KATA YA MWANGATA

Diwani viti maalum Manispaa ya iringa kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)Leah Mleleu akizungumza na akina mama wa Kata ya mwangata
Diwani viti maalum Manispaa ya iringa mjini Leah Mleleu Leo tar 17.7.2017

Amekutana na wakimama Wajasiliamali wa Kata ya Mwangata

Mh diwani Amekutana Wa kimama walionufaika na Mikono inayotolewa na halmshauli ya manispaa ili kujua maendeleo ya shughuli zao za ujasiliamali Pamoja na changamoto zao

Pili Mh diwani amekutana Pia na kina mama wajasiliamali Ambao hajajiunga kwenye vikundi na kuwaomba wajiunge kwenye vikundi ili waweze kunufaika na mikono inayotolewa na halmshauli 5% kwa ajili Ya wakina mama na vijana

Mlitupigania sisi chadema na sasa mmetupa halmshauli Nawaombeni Mchangamkia fursa kwa kuunda mikundi ili muweze kukopesheka,Sisi kama halmshauli tutatao mikopo bila kujali itikadi ya chama,dini wala rangi ya mtu zaidi

baadhi ya kina mama wajasiliamali walimshukuru mh diwani vitu maalum kwa kutenga muda wake na kukutana nao,Pamoja na kuweelimisha namna ya kunufaika mikopo ya kina mama inayotolewa na halmshauli,Kwa sababu walikuwa hawana uelewa wowote 

Na kuhaudi endapo watafanikiwa kupata mikopo hiyo wataitumia kutokana na madhumuni yaliyowekwa kwa mjibu wa sheria na kanuni

Mh diwani aliongozana na Katibu Bavicha mkoa Jackson Mnyawami

Oscar Mgaya ni mratibu mhamasishaji bavicha manispaa

Kwa Pamoja walipongeza mh diwani viti maalum kwa kuwatembelea wakina mama Na  halmshauli ya manispaa ya iringa kwa ujumla kwa kutoa mikopo kwa vijana na kina mama wajasiliamali  

kwani kutasaidie wananchi kujikomboa na umasikini

Imetolewa na 

Oscar Mgaya

Mratibu wa ziara
18.07,2017

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More