Sunday, May 7, 2017

VYUO NA SHULE ZA MAKANISA MKOANI IRINGA KUFUNGWA

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati akizungumza na viongozi pamoja na vijana wa Kabisa la kikatoliki jimbo la Iringa wakati wa Mashindano ya kuimba na kucheza ngoma yaliyofanyika katika palokia ya Kihesa
padri Emily Kindole ambaye ni mshauri wa vijana wa vikaria vya iringa consolata wakati wa mashindano ya kuimba nyimbo za injili kwa vijana vikaria wa kanisa la katoliki jimbo la Iringa linalojumuisha vikaria kumi na mbili kutoka kanda zote.

Na Fredy Mgunda, Iringa.

Vyuo na shule za makanisa mkoani Iringa zipo mbioni kufungwa kutokana serikali kuyataka makanisa kuendesha vyuo na shule kibiashara tofauti na walivyozea kutoa huduma kwa jamii ambazo zinawazunguka.

Hayo yamezungumzwa na padri Emily Kindole ambaye ni mshauri wa vijana wa vikaria vya iringa consolata wakati wa mashindano ya kuimba nyimbo za injili kwa vijana vikaria wa kanisa la katoliki jimbo la Iringa linalojumuisha vikaria kumi na mbili kutoka kanda zote.

Padri Kindole alisema kuwa wamepata maagizo kutoka serikalini yakiwataka kuendesha vyuo na shule kibiashara wakati makanisa yamekuwa yakifanya kazi za kijitolea kwa jamii hivyo hawapo tayari kuendesha au kufanya biashara yoyote.

"Makanisa hayajawi kufanya biashara na hayapo tayari kufanya biashara kwa kuwa lengo la kanisa ni kutoa huduma kwa jamii kwa kuwa tumepata maagizo kutoka serikalini hivyo tutalazimika kuzifunga kwa kuwa hatuwezi kuendesha vyuo na shule zetu kwa Biashara"alisema Kindole

Padri Kindole alimtaka mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati wa chama cha mapinduzi CCM kupeleka kilio chao bungeni ili kuzifanya shule na vyuo ya makanisa zisifungwe kwani wakifanya biashara makinisani kitakuwa kinyume cha maagizo ya mwenyezi mungu.

Lakini pia Padri Kidole aliwataka vijana wa vikaria vyote kujikitaka kwenye elimu ya aina yoyote ili kuwafanya wapate maalifa yatakayo wasaidia katika maisha yao ya baadae.

"Kijana ukiwa huna elimu huwezi kuwa na maarifa ya hali ya juu ni lazima kuikimbilia elimu ili kuendana na teknologia iliyopo sasa bina kuwa na elimu utapitwa na vitu vingi hata hivyo utamuungasha Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John pombe Magufuli kuifanya Tanzania ya viwanda" alisema Padri Kindole

Aidha Padri Kindole aliwataka vijana wa kujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI kwa kuwa unamaliza vijana wengi na kupunguza nguvu za taifa na kulifanya taifa kuwa vijana dhaifu na kulirudisha nyuma taifa kwenye maendeleo.

Kwa upande wake mgeni rasmi mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati wa chama cha mapinduzi CCM alisema kuwa azipokea changayza vyuo na shule za makanisa na kusema kuwa ameanza kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na viongozi wa vyuo vikuu wote wa Mkoani Iringa na tayari swala hilo lipo bungeni linaendelea vizuri.

Kabati aliwataka viongozi wa dini zote kuwa na subila wakati swala hilo linashughulikiwa kwa kuwa limeshafika bungeni na kamati husika zinalishughulikia kwa umakini na wakati wa bajeti ya elimu majibu yanaweza patikana.

"Tulienda kwenye kamati mbili tofauti kulifikisha swala hili na tayari maprofessa kutoka vyuo vikuu vya hapa mkoani walikutana na kamati na waliwasilisha mapendekezo yao na nafikiri wanayafanyia kazi kwa kuwa tatizo hili sio Iringa tu ni la nchi nzima"alisema Kabati

Kabati alisisitiza ili kuwa na serikali ya viwanda ni lazima vyuo vya ufundi vipewe kipaumbe kwa lengo la kuzalisha wanyakazi bora kwenye viwanda mbalimbali,vyuo vya VETA peke yake haviwezi kuzalizalisha wanafunzi wa kutosha kuhudumia viwanda vyote hivyo ni lazima kuvijali vyuo vyote hata nchini.

Naye Josiah Kifunge msaidizi wa mbunge wa viti maalum ritta kabati wa CCM aliwataka vijana kujiepusha na maswala ambayo hayana umuhimu kwa maendeleo ya taifa hasa vijana wengi kutumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kufanya kazi.

"Unamkuta kijana kwa siku anatumia zaidi ya masaa kumi kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, Twitter na snap chat hivyo unakuta akili zao zipo huko na sio kufikilia jinsi gani kuijipatia kipato sasa kwa namna hiyo hatuwezi kuendesha nchi yetu kuelekea serikali ya viwanda"Kifunge

Kifunge aliwaomba vijana kutokata tama badala yake kutafuta fursa za kutatua changamoto zinazowakabili na mara nyingine kutafuta njia za kujiajili kuliko kitegemea ajira kutoka serikalini au kwenye mashirika binafsi.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More