Tuesday, May 30, 2017

CHUMI AITAKA WIZARA YA MAMBO YA NJE KUPELEKA MAAFISA KWENYE BALOZI

Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi ameitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuharakisha mchakato wa kupeleka maafisa kwenye Balozi zetu ili kuhakikisha utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi.

Chumi alisema kuwa ili kuelekea uchumi wa viwanda ni muhimu ofisi za Kibalozi zijajengewa uwezo ili kufanya kazi kwa ufanisi. 

'hadi ninapozungumza Balozi kumi na tano hazina Maafisa wa kuwasaidia Mabalozi, hali inayofanya mazingira magumu ya kutekeleza majukumu yao' alisisitiza Mbunge huyo ambaye amewai kufanya kazi katika Wizara hiyo. 

Akifafanua, Chumi alisema kuwa kuwaacha Mabalozi katika nchi kubwa China kufanya kazi bila wasaidizi ni kufifisha jitihada za kuelekea uchumi wa Viwanda kwa kuwa tunategemea tupate wawekezaji kutoka nchi hiyo.

'Ubalozi wa Brussels ambako ni makao makuu ya Jumuiya ya Ulaya kuna mikutano mingi sana, sasa Balozi anapokuwa hana maafisa inamkosesha fursa ya kushiriki mikutano hiyo na hivyo kama Taifa tunajikuta tunakosa fursa nyingi' alisisitiza na kuongeza kuwa

Balozi wetu wa Berlin, Ujerumani anawakilisha zaidi ya nchi saba, anapofanya kazi bila maafisa hawezi kutekeleza majukumu ipasavyo. 

Aidha Mbunge huyo wa Mafinga Mjini alifafanua kuwa unapokosa maafisa ni sawa na ku-down size suala ambalo ni kama ku-down grade mahusiano. 

Wabunge wengine waliochangia hoja hiyo wakiwemo Tundu Lisu, Joseph Kakunda na Dr Faustine Ndungulile walipongeza hatua za kuwarejesha maafisa waliokaa lakini wakaeleza kuwa hatua hiyo lazima iendane na kuwapeleka haraka maafisa katika Balozi zetu. 

Akijibu hoja hiyo Naibu Waziri Dk. Suzan Kolimba alikiri kuwa hoja ya Chumi ni ya Msingi na kwamba tayari fedha zimetingwa kuwapeleka maafisa katika mwaka huu wa fedha.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More