Wednesday, May 24, 2017

CHUMI AITAKA SERIKALI KUZINGATIA UHIFADHI NA USTAWI WA MAISHA YA WATU.

Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi ameishauri serikali kuzingatia uhifadhi unaojali ustawi wa maisha ya watu ili kuondokana na migogoro isiyo ya lazima. 

Chumi aliyasema hayo wakati akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya maliasili na utalii. 

'Uhifadhi wa zama hizi ni ule tunaoita UHIFADHI NA MAENDELEO YA WATU  yaani Conservation with development, Sasa huwezi kuzungumzia uhifadhi unaoathiri maisha ya watu, unazuia watu wasilime vinyungu, unazuia mifugo, je uhifadhi huo ni kwa manufaa na faida ya nani' alihoji Mbunge huyo.

Akizungumzia hatua ya serikali kuwataka watu wenye misitu binafsi kupata kibali kwanza ndipo waruhusiwe kuvuna misitu Yao binafsi, alisema hilo haliwezekani.

'Hivi mtu ana shida, labda mtoto amekosa mkopo wa elimu ya juu, au anauguliwa , eti mpaka watu wa misitu wakague ndipo wamruhusu kama miti imefikia umri wa kuvuna, hilo halikubaliki' na kuongeza mara vinyungu, mara mashart ya mtu kujivunia miti yake, je mlimpa miche,  alihoji. 

Aidha alihoji kwanini tunawauzia MPM nusu ya bei kwa kigezo cha kuwa ni mwekezaji na tunawakandamiza wawekezaji wazawa.

"Jambo hili niligusia mwaka Jana, kwanini mnawajali wawekezaji wa nje na kuwapuuza wazawa "

Kuhusu utalii, Chumi alisisitiza kuwa ni lazima kuipa nguvu Bodi ya Utalii hasa katika kutangaza. Akitoa mfano alisema kuwa Uganda walitenga dola milioni nane ($ 8m) na Rwanda dola milioni 11 ($11m) za kimarekani kwa bajeti Yao ya 2016/17 kwa ajili ya kutangaza utalii, wakati Kenya walitumia dola 3.9 za kimarekani kutangaza katika soko moja tu la Italia kwenye maonyesho ya barabarani ya Italy Expo, wakati Sisi tumeitengea TTB dola milioni mbili tu ($2m).

Akigusia umuhimu wa kuwa na mpango bora wa matumizi ya ardhi Chumi alisema kuwa wakati Vietnam yenye eneo la kilometa za mraba 360,000 ina watu milioni tisini na uwiano wa watu 255 kwa kilometers square,  Tanzania yenye kilometa za mraba 900,000 ina watu milioni hamsini na tatu na uwiano wa watu 57 kwa kilometers square, Singapore watu 7600 kwa kilometer square akini tunagombana kila siku Kuhusu wafugaji  na wakulima, 

'Ni vizuri Sasa tukaja na mpango wa matumizi bora ya ardhi kwa kushirikiana Wizara zote zinazoguswa na suala hili'.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More