Wednesday, May 31, 2017

MAKUMI WAFUNGULIWA KWENYE MKUTANO WA OYES 2017 JIJINI MWANZA.

Makumi ya wakazi wa Jiji la Mwanza na viunga vyake waliohudhuria kwenye mkutano wa Injili wa OYES 2017 (Open Your Eyes and See) jana wamefunguliwa na kumpokea Kristo. Kabla ya kuanza mkutano huo, Mchungaji Garry White (kushoto) kutoka Marekani alitoa semina kwa akina mama, vijana na wanandoa ambapo tamati ya mkutano huo unaofanyika viunga vya Kanisa la EAGT Lumala Mpya, nyumba ya Soko Kuu la Sabasaba Jijini Mwanza ni jumapili June 04,2017. Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Kulola, amewasihi watu wote kuhakikisha wanahudhuria mkutano huo uliojaa mahubiri na mafundisho ya neno la Mungu yakilenga kumfungua kila mmoja ili kuuona Ukuu na Utukufu wa Mungu. #BMGHabari Mchungaji Garry White kutoka Marekani akihudumu kwenye...

TBS YAWASHAURI WAZALISHAJI WADOGO WADOGO WA BIDHAA KUTUMIA FURSA YA BURE YA UKAGUZI

Wazalishaji wadogo wadogo wa bidhaa nchini wameshauriwa kutumia fursa ya bure ya ukaguzi wa bidhaa zao inayotolewa na Shirika la Viwango Tanzania TBS. Hayo yamesemwa na Afisa Masoko Mwandamizi kutoka katika shirika hilo,Gladnes Kaseka pichani kushoto juu wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya tano ya biashara ya Mkoa wa Tanga . Alisema kuwa licha ya TBS kutoa fursa hiyo lakini bado wazalishaji wadogo na wakati wameshindwa kuitumia fursa hiyo kwa ukamilifu wake na kusababisha kuendelea kuwepo kwa bidhaa ambazo hazina nembo ya ubora. "Bado wazalishaji wetu wengi hawajaweza kuifikia fursa hiyo ambayo itaweza kuwasaidia kuhakikisha wanazalisha bidhaa zenye ubora lakini wataweza kuingiza bidhaa zao kwa urahisi...

WAANDISHI WA HABARI ZA KILIMO TANZANIA (TAJF) WAKUTANA MALAIKA BEACH RESORT JIJINI MWANZA KUPANGA MIKAKATI

 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Kilimo Tanzania (TAJF), Gerald Kitabu (kulia), akizungumza na waandishi wa habari wanachama wa TAJF wakati wa kikao kilichofanyika Ufukwe wa Malaika Beach Resort jijini Mwanza jana kujadili masuala mbalimbali ya chama hich...

MWENGE WA UHURU KUWASILI WILAYA YA UBUNGO KESHO 31 MEI 2017

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Kibamba Chama-Dar es salaam Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori akizungumza na Waandishi wa habari Mwenge wa Uhuru Mwaka 2017 utawasili kesho Tarehe 31 Mei 2017 katika Wilaya ya Ubungo kuanzia saa moja kamili asubuhi na kuzuru katika Miradi mitano ya Maendeleo.          Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori amesema kuwa katika mbio hizo za Mwenge wa Uhuru Mradi mmoja wa kituo cha Polisi Gogoni utawekwa jiwe la msingi. Alisema kuwa Miradi mingine itakayozinduliwa ni Mradi wa Ujenzi wa Jengo la kutolea huduma za VVU katika...

MATUKIO MBALIMBALI KWENYE MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA JIJINI TANGA

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kushoto akitoa elimu kuhusu umuhimu wa wananchi kujiunga na mfuko huo kwa wakazi wa Jiji la Tanga kwenye banda lao lililopo katika eneo la Mwahako Jijini Tanga kunakofanyika maonyesho ya tano ya biashara ya kimataifa  Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage akiptia kwenye banda la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) wakati alipofungua maonyesho ya kimataifa ya  biashara ya tano yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga  Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage akisalimiana na mmoja wa watumishi Tanapa wakati wakati alipotembelea banda lao kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella  Waziri...

Tuesday, May 30, 2017

CHUMI AITAKA WIZARA YA MAMBO YA NJE KUPELEKA MAAFISA KWENYE BALOZI

Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi ameitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuharakisha mchakato wa kupeleka maafisa kwenye Balozi zetu ili kuhakikisha utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi. Chumi alisema kuwa ili kuelekea uchumi wa viwanda ni muhimu ofisi za Kibalozi zijajengewa uwezo ili kufanya kazi kwa ufanisi.  'hadi ninapozungumza Balozi kumi na tano hazina Maafisa wa kuwasaidia Mabalozi, hali inayofanya mazingira magumu ya kutekeleza majukumu yao' alisisitiza Mbunge huyo ambaye amewai kufanya kazi katika Wizara hiyo.  Akifafanua, Chumi alisema kuwa kuwaacha Mabalozi katika nchi kubwa China kufanya kazi bila wasaidizi ni kufifisha jitihada za kuelekea uchumi wa Viwanda kwa kuwa tunategemea tupate wawekezaji kutoka nchi hiyo. 'Ubalozi wa Brussels...

Friday, May 26, 2017

DC UBUNGO MHE KISARE AAGIZA KUAZNZA MCHAKATO WA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI KATA YA KIMARA

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na wananchi mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori (Kulia), Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota wakikagua eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017 Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Kimara wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori wakati akizungumza nao mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017 Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota akizungumza na wananchi wa Kata hiyo...

CCM YAMPONGEZA JPM SAKATA LA MCHANGA WA MADINI, YALAANI VIKALI MAUAJI MKOANI PWANI

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Itikadi na Uenezi Ndg Humprey Polepole akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam. Picha Zote na Mathias Canal Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Itikadi na Uenezi Ndg Humprey Polepole akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam. Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Itikadi na Uenezi Ndg Humprey Polepole wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Mikutano Ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijini Dar es salaam. Katibu wa Halmashauri Kuu ya...

BURUDANI ZA GULIO LA MTAA KUTOKA LAKE FM MWANZA ZAANZA KWA KISHINDO

DJ Buster kutoka Lake Fm akisababisha burudani kweny Gulio la katika Mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza. 102.5 Lake FM Mwanza, #RahaYaRockCity #RedioYaWananzengo leo Mei 26,2017 imezindua rasmi burudani za Gulio la Mtaa kupitia kampeni yeke ya usafi ya Ng'arisha Nzengo Uchafu Nuksi. Burudani leo iko katika mnada wa Nyakato National Jijini Mwanza kisha itahamia kwenye minada yote Jijini Mwanza ambapo kuna makumi ya wasanii watakaoshusha burudani kali balaa. Kupitia burudani, Lake Fm inahamasisha suala la usafi minadani na mkoani Mwanza kwa ujumla. Pia kila mnada atatafutwa Mama Lishe Bora, Balozi Imara na Mwananzengo Hodari ambapo watajipatia zawadi. Burudani za Gulio la Mtaa zimepewa nguvu na Pepsi, Tigo, Busy Bee, Barmedas...

Page 1 of 69412345Next
Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More