Thursday, February 26, 2015

MTOTO MCHANGA AUAWA NA KUTUPWA KICHAKANI MKOANI MOROGORO

Matukio ya kutupa watoto wachanga yameendelea mkoani Morogoro ambapo mtoto mchanga wa siku moja ameuwa na kutupwa vichakani katika eneo la kichangani mjini Morogoro.

Mtoto huyo mwenye jinsi ya kike anaonekana ametupwa kwa saa kadhaa zilizopita ambapo wakizungumzia tukio hilo baadhi ya mashuhuda wamelalamikia kuongezeka kwa matukio ya watoto wachanga kutupwa  ambapo wameomba wazazi kuwahurumia watoto   wasio na hatia huku baadhi ya wakinamama waliokuwepo katika tukio hilo wameonyesha kusikitishwa na kueleza wakati mwingine inatokana na baadhi ya wanaume kukwepa majukumu.
 
Naye mwenyekiti wa mtaa na diwani wa kata ya kichangani John Waziri walioshuhudia tukio hilo wamesema tukio hilo si la kuvumilika na kuomba wananchi kuwafichua wanaowabainika kuzaa na kutupa watoto  kwa lengo la kukwepa majukumu na pia kuomba wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kufanikisha kupatikana kwa mtuhumiwa.
 
Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na wamefika katika eneo la tukio na kuchukua mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More