skip to main
|
skip to sidebar
Home
Home
About us
News
National News
International News
Business and Economics News
Sports and Entertainments News
Contact us
Wednesday, February 25, 2015
FFU watumia mabomu kutuliZa vurugu Ilula ,magari yachomwa moto ,mahabusu waachiwa silaha zaporwa
Wednesday, February 25, 2015
mwangaza wa hbari
No comments
Email This
BlogThis!
Share to X
Share to Facebook
Askari wa FFU wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kutuliza vurugu kubwa zilizoibuka leo Kati ya Polisi na wananchi wa mjini wa Ilula katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa kufuatia kifo chenye utata cha mwanamke mmoja
Tukio hilo limetokea majira ya saa 5 asubuhi Leo na kudumu hadi Majira ya saa 10 jioni huku kituo cha Polisi kikivunjwa ,bunduki kuporwa na nyingine kuchomwa moto pamoja na magari matatu na Pikipiki Moja ya polisi.
Wakielezea tukio hilo wakazi wa mji wa Ilula wameueleza mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz kuwa chanzo ni askari watatu watatu akiwemo mkuu wa kituo cha Ilula kwenda kufanya msako wa wananchi wanaokunywa pombe muda wa kazi.
Hivyo kutokana na tukio hilo mwanamke huyo aliyepoteza Maisha aliyetambulika kwa jina la Mwanne Mtandi aliamua kukimbia kukwepa kukamatwa na Polisi hao Kabla ya kukutwa nyuma ya jengo la klabu hicho cha pombe za kienyeji kilichopo mtaa wa Ilala Mjini Ilula akiwa amekufa.
" Polisi hawa kila siku wamekuwa wakifika hapa klabuni na kukamata watu na siku kwanza walimkamata marehemu na kumtoza faini ya Tsh 20,000 na siku ya pili walimkamata yeye na mumewe na kuwatoza faini Tsh 40,000 na leo walikuwa wakija kumkamata tena na hapo ndipo mwanamke huyo aliamua kutimua mbio Kabla ya kukutwa amekufa" alisema shuhuda wa tukio hilo Shida Ngwata.
Huku Mkazi mwingine ambae hakutaka jina lake kutajwa hapa alisema kuwa Polisi hao walilazimika kutumia mabomu na risasi za moto kutokana na umati mkubwa wa watu waliojitokeza huku Moja Kati ya bomu likiokotwa ambalo lilikuwa halijalipuliwa.
Alisema kuwa askari watatu watatu ndio ambao walikuwa wakisakamwa na Raia hao ambao pia wamevunja vioo vya basi la Upendo kufuatia mkuu wa kituo Ilula kukimbilia ndani ya basi hilo wakati akifukuzwa na Raia hao .
Diwani wa kata ya Nyalumbu Ally kikunga alisema kuwa alipigiwa simu na wananchi wake kujulishwa juu na vurugu hizo na Baada ya kufika Eneo la tukio alikuta mwanamke huyo akiwa mahututi ila hakuweza kupata msaada toka kwa wananchi wengine ila kumkimbiza hospitali .
Diwani huyo alilishauri jeshi la Polisi kuacha kutumia nguvu zaidi Kwani alisema Eneo hilo la klabu ni Eneo ambalo pia wananchi wanapata mahitaji mbali mbali na kuwa mwanamke huyo alikuwa akifanya usafi katika chumba chake cha biashara ya pombe.
Hata hivyo alisema Raia hao wameharibu Mali mbali mbali pamoja na nyaraka zote na kuwafungulia mahabusu wote waliokuwemo mahabusu huku Lori Moja lililokamatwa kituoni hapo likilindwa kuharibiwa kuwa halina kosa.
Vurugu hizo zilisababisha wasafiri wanaotumia barabara ya Kuu ya Mikoa ya Nyanda za juu kusini kukwama kwa zaidi ya masaa 6 .
Kaimu mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya kilolo ilifika eneo la tukio na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiahidi kutoa taarifa kamili ya Mali zilizoharibiwa na chanzo halisi cha tukio hilo Baada ya kukaa kikao na viongozi wa jeshi na Polisi na wale wa mji wa Ilula
Japo mwandishi wa habari hizi alishuhudia magari mawili ya Polisi na Pikipiki yakiwa yamechomwa moto ,gari Moja la askari pia lilichomwa moto na magari mawili Moja la askari na daladala moja na basi la upendo kuharibiwa vibaya
Newer Post
Older Post
Home
0 comments:
Post a Comment
Popular Posts
Tamko la Jukwaa la Wahariri kuhusu kufutwa kwa gazeti la MAWIO
UTANGULIZI 1. JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limeshtushwa na kusononeshwa na hatua ya Serikali kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamadu...
ZIJUE AINA TANO ZA MITUNGI YA KUZIMIA MOTO
1.MTUNGI WA MAJI(WATER) Mtungi huu una rangi NYEKUNDU wote. Mtungi huu hautumiki kuzimia moto wa umeme au mafuta, ila unazima aina nyingi...
Kamati ya Bunge yatua Rock City Mall, kuna jambo imelibaini
Kamati ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa leo imefanya ziara katika jengo la kitega uchumi la Rock City Mall ili kujionea utekeleza...
MJI MKONGWE WA ZANZIBAR: PALE DUNIA YA KALE INAPOKUTANA NA YA KISASA
Na Jumia Travel Tanzania Miongoni mwa majengo yake mengi yakiwa yamejengwa mnamo karne ya 18 na 19, Mji Mkongwe wa Zanzibar bado hau...
WANAFUNZI WALIOHITIMU DARASA LA SABA 1993 SHULE YA MSINGI NYAKATO JIJINI MWANZA WAIKUMBUKA SHULE YAO.
Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kushoto), wakimkabidhi Afisa...
CHUO CHA AFRICA GRADUATE UNIVERSITY CHAWATUNUKU PhD WANAOFANYA KAZI ZA JAMII NCHINI
Mkuu wa Chuo cha Africa Graduate University cha jijini Dar es Salaam, Profesa Stiven Nzowa, akiongoza mahafali ya kuwatunuku Tuzo ya Hes...
Wanahabari watakiwa kuacha kuamini kila kitu, wasome
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akisheheresha kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya radi...
KALIDUSHI MWENYEKITI MPYA WA CCM MKOA WA GEITA
Wajumbe wakiwa wamembeba mshindi wa kiti cha uenyekiti Mkoani Geita,Alhaji Said Maneno Kalidushi baada ya kuibuka mshindi kwa kura 358. ...
MHE MWANJELWA AWATAKA WAJUNBE MKUTANO MKUU CCM MKOA WA MBEYA KUCHAGUA VIONGOZI MAKINI
Naibu Waziri Wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza na wajumbe wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)...
WAFANYAKAZI JUMIA WAFANYA MATEMBEZI YA HISANI KUCHANGIA FEDHA KUSAIDIA JAMII
Na Jumia Travel Tanzania Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka mitano tangu Jumia ianze kufanya shughuli zake barani Afrika, wafany...
Categories
Habari za jamii
Habari zote
Siasa
Videos
Blog Archive
►
2025
(23)
►
November
(2)
►
October
(4)
►
September
(8)
►
July
(1)
►
June
(3)
►
May
(4)
►
April
(1)
►
2024
(1)
►
March
(1)
►
2023
(1)
►
October
(1)
►
2021
(2)
►
July
(1)
►
June
(1)
►
2018
(249)
►
June
(9)
►
May
(16)
►
April
(36)
►
March
(67)
►
February
(60)
►
January
(61)
►
2017
(1008)
►
December
(81)
►
November
(125)
►
October
(166)
►
September
(80)
►
August
(109)
►
July
(51)
►
June
(37)
►
May
(57)
►
April
(78)
►
March
(89)
►
February
(61)
►
January
(74)
►
2016
(1104)
►
December
(54)
►
November
(47)
►
October
(74)
►
September
(125)
►
August
(88)
►
July
(67)
►
June
(60)
►
May
(72)
►
April
(102)
►
March
(108)
►
February
(152)
►
January
(155)
▼
2015
(410)
►
December
(113)
►
November
(160)
►
October
(89)
►
September
(1)
►
August
(2)
►
July
(6)
►
June
(7)
►
May
(5)
►
April
(4)
►
March
(12)
▼
February
(11)
MTOTO MCHANGA AUAWA NA KUTUPWA KICHAKANI MKOANI MO...
UKAWA WAITAKA SERIKALI KUSITISHA ZOEZI LA UPIGAJI ...
JESHI LA POLISI LAPATA AIBU KUBWA, POLISI WAKE AKU...
SERIKALI ISIMAMIE VYEMA HAKI ZA BINADAMU KWA KUSHI...
FFU watumia mabomu kutuliZa vurugu Ilula ,magari y...
KIJANA WA KITANZANIA AUNDA REDIO STESHENI
WATANZANIA WAASWA KUTHAMINI BIDHAA ZINAZOZALISHWA ...
CHAMA CHA ALBINO KUMSHITAKI RAIS KIKWETE UMOJA WA ...
MTANDAO WA HAKI ZA BINADAMU WATOA TAMKO JUU YA KUT...
TAMWA YATOA MAFUNZO KWA WANAHABARI WA MIKOA YA NYA...
JAY Z NA MTOTO NJE YA NDOA
adv1
0 comments:
Post a Comment