Thursday, February 26, 2015

UKAWA WAITAKA SERIKALI KUSITISHA ZOEZI LA UPIGAJI KURA YA MAONI YA KATIBA PENDEKEZWA

Viongozi wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA umeitaka serikali kusitisha zoezi la upigaji wa kura ya maoni ya katiba kutokana na zoezi hilo kutokidhi vigezo vya kisheria na badala yake ielekeze nguvu na rasilimali fedha katika zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ili kuliepusha taifa kuingia katika machafuko.

Viongozi wakuu wa vyama vinavyounda umoja huo wa katiba ya wananchi ukawa wakiongozwa na Profesa Ibrahimu Lipumba wa chama cha wananchi CUF na Freeman Mbowe wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema, chama cha NLD Dr Emmanuel Makaidi, chama cha NCCR mageuzi Mosena Nyambabe wameitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari.
 
Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahimu Lipumba amemtaka rais Prof Jakaya Mrisho Kikwete kutoa kauli ya kuusitisha mchakato wa kura za maoni ya katiba pendekezwa kwa kuwa zoezi hilo kwa sasa haliwezi kutekelezeka April 30 ya mwaka huu kama rais alivyotangaza licha ya kutokuwa na mamlaka ya kutangaza tarehe ya kufanyika kwa kura hizo za maoni.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Freeman Mbowe ameitaka serikali kuelekeza fedha kidogo zilizopo katika zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kuwa zoezi hilo linakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vifaa vya kutosha na kusitisha kabisa zoezi la kura za maoni ya katiba ili kuiepusha nchi na kile alichodai kuwa ni machafuko yanayowea kuzuilika.
 
Hivi sasa taifa liko katika maandalizi ya kushiriki katika zoezi la kura za maoni ya katiba pendekezwa linalotarajiwa kufanyika alhamis ya April 30, 2015 kama ilivyotangazwa na mh rais wa jamhuri ya mungano wa Tanzania licha ya uwepo wa kauli za kulipinga zoezi hilo kutoka hasa katika vyama vya siasa vya upinzania na baadhi ya vyama vya kiraia kwa sababu kadha wa kadha

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More