Tuesday, June 5, 2018

Chumi ashikilia shilingi kuitaka Serikali kutoa fedha za Miradi Viporo kama ilivyoahidi, Spika aokoa jahazi

Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi ameitaka serikali kutoa fedha za miradi viporo kama ilivyoahidi kwa kuwa mwaka wa fedha unaelekea mwishoni. Chumi alitoa hoja hiyo wakati Bunge limekaa kama Kamati kujadili bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango ambapo alisema kuwa, ni Serikali yenyewe ndio ilizitaka Halmashauri kuwasilisha miradi viporo ambayo mingi ilitokana na nguvu za wananchi. Akijibu hoja hiyo, Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Ashantu Kijaji alisema kuwa Serikali inafanya uchambuzi wa miradi hiyo ndipo itoe fedha. Hata hivyo, Chumi alihoji ni uchambuzi gani ikiwa miradi hiyo ilianishwa na kuchambuliwa kwa ushirikiano kati ya Halmashauri na Tamisemi. Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi upi huo ambao serikali inaufanya ikiwa Halmashauri...

Monday, June 4, 2018

MKURUGENZI WA NGOTI GREEN ACADEMY AWATAKA WAZAZI KUWALEA WATOTO KIMAADILI

 Mkuu wa shuleya Ngoti Green Academy  Jonson Mtewele kushoto akiwa na mkurugunzi wa Ngoti Green Academy Thomas Ngoti ambaye alikuwa anatoa neno kwa wazazi waliofika kwenye kikao cha pamoja baina ya wazazi walimu na wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo  Mmoja wa wazazi walifika katika shule ya Ngoti Green Academy akitoa neno mbele ya wageni waalikwa na mkurugunzi wa Ngoti Green Academy Thomas Ngoti  Picha za pamoja baina ya wazazi,walimu na viongozi wa shule ya Ngoti Green Academy   Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Ngoti Green Academy  NA FREDY MGUNDA,IRINGA Mkuu wa shule ya Ngoti Green Academy  amewataka wazazi na walezi mkoani Iringa kuwalea watoto katika maadili yanayostahili...

UMEME NI NISHATI MBADALA ILIYO NAFUU KWA MATUMIZI YA NYUMBANI: KAMOTE

 Bw. Ally M. Koyya, (kulia), kutoka idara ya Masoko TANESCO, akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea kwenye banda la Shirika hilo kwenye maonesho ya Nishati Mbadala yanayokwenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam Juni 4, 2018. NA K-VIS BLOG/Khalfan Said SHIRIKA la Umeme Nchini (TANESCO) limesema hakuna sababu yoyote kwa wananchi kuogopa kutumia nishati ya umeme kwa matumizi mbalimbali ya nyumbani kwani ni nafuu mno ukilinganisha na nishati nyingine. Afisa Mazingira wa Shirika hilo, Bw.Yusuf Kamote, amesema hayo kwenye maonesho ya Nishati mbadala ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani yanayoendelea kwenye viwanja...

VIONGOZI 11 WA UPINZANI WARUSHIWA KOMBORA LA UFISADI ZITTO KABWE ATAJWA KUWA NI NAMBA MOJA

 Mwanasheria Patrobas Katambi. Mwenyekiti mstaafu wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA), ambaye kwa sasa ni kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mwanasheria Patrobas Katambi, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu viongozi wa upinzani kujinufaisha kupitia elimu na vyeo vyao. Soma taarifa hiyo hapa chini. TUHUMA NZITO ZISIZOKANUSHIKA ZINAZOWAKABILI VIONGOZI WA UPINZANI KUJINUFAISHA KUPITIA ELIMU NA VYEO VYAO. Ndugu, Watanzania na Ndugu Waandishi wa habari, Asasi za Kiraia na Taasisi zote wadau wa Maendeleo Tanzania, nawasalimu kwa Jina la Amani.  Nchi yetu tumepewa na Mungu, utajiri wa Rasilimali za kila aina, ila Watu wake ni Masikini...

MANENO YA MWISHO YA MAPACHA WALIOUNGANA KABLA HAWAJAKATA ROHO

“DAKTARI tunakufa” yalikuwa ni maneno pekee yaliyotolewa ndani ya dakika 15 na Consolata Mwakikuti baada ya kushuhudia pacha mwenzake Maria Mwakikuti akitangulia kukata roho katika tukio la kusikitisha lililotokea mjini Iringa juzi. Pacha hao walioungana ambao habari zao zilikuwa gumzo katika vyombo mbalimbali vya habari toka udogo wao hadi sasa, walifariki majira ya saa 2.30 na saa 3.00 usiku wa Jumamosi wakiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa waliokokuwa wakiendelea na matibabu. Akizungumza na wanahabari jana mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Museleta Nyakirito alisema pacha hao walikuwa na tatizo kwenye njia ya hewa hatua iliyosababisha wafikwe na mauti. Dk Nyakirito alisema Maria alikuwa wa kwanza kufa...

Sunday, June 3, 2018

RAIS MAGUFULI KUZINDUA PROGRAMU YA KUENDELEZA SEKTA YA KILIMO AWAMU YA PILI (ASDP II)

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (Katikati) akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo (ASDP II) katika jengo la Mikutano la kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam, jana 1 June 2018. Wengine ni Katibu Mkuu wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu wizara ya kilimo Dkt. Thomas kashililah. Picha zote Na Mathias Canal-WK Wawakilishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakifatilia mkutano wa Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba katika jengo la Mikutano la kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam, Jana 1 June 2018. Katibu Mkuu wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (Kulia),  Mratibu...

Saturday, June 2, 2018

NAIBU WAZIRI JULIANA SHONZA MGENI RASMI TAMASHA LA TAGOANE ARUSHA

Na Mwandishi wetu, Arusha Mtandao wa Wasanii wa Injili na Maadili ya Utaifa Tanzania (Tagoane) umeandaa tamasha kubwa la ‘Tanzania Mama Niwathamani’ linaloitwa Tamani Festival "Asante Mama" lenye lengo la kumshukuru Mungu kwa ajili ya Mwanamke(Mama), kuonyesha thamani ya mama (Mwanamke) na kurejesha shukrani kwa mama kutokana na umuhimu wake kwenye jamii. Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa Tagoane Dkt. Godwin Maimu alisema tamasha hilo litakalofanyika June 29-Julai mosi jijini Arusha litawashirikisha watu wengi wakiwamo wanamuziki wa Injili. Alisema lengo hasa ni kurejesha shukrani kwa ‘mama’ Asante Mama ambapo pamoja na mambo mengine, watu watachangia damu salama kwa ajili ya kuokoa uhai wa mama na mtoto wakati wa kujifungua. Dkt....

Friday, June 1, 2018

WANAKIJIJI 772 WA KIJIJI CHA MLANDA WAPATA HATI MILIKI ZA KIMILA 1,777

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya na naibu mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki Msigwa wakimkabidhi hati ya kimila mmoja ya wananchi wa kijiji cha Mlanda ambaye ni mlemavu   Naibu mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki Msigwa akitoa neo kwa wananchi wa kijiji cha Mlanda wakati wa kutoa hati za kimila   Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya na naibu mkurugenzi wa Mradi wa...

Page 1 of 69412345Next
Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More