
Mbunge wa Mafinga Mjini Cosato Chumi ameitaka serikali kutoa fedha za miradi viporo kama ilivyoahidi kwa kuwa mwaka wa fedha unaelekea mwishoni.
Chumi alitoa hoja hiyo wakati Bunge limekaa kama Kamati kujadili bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango ambapo alisema kuwa, ni Serikali yenyewe ndio ilizitaka Halmashauri kuwasilisha miradi viporo ambayo mingi ilitokana na nguvu za wananchi.
Akijibu hoja hiyo, Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Ashantu Kijaji alisema kuwa Serikali inafanya uchambuzi wa miradi hiyo ndipo itoe fedha.
Hata hivyo, Chumi alihoji ni uchambuzi gani ikiwa miradi hiyo ilianishwa na kuchambuliwa kwa ushirikiano kati ya Halmashauri na Tamisemi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, uchambuzi upi huo ambao serikali inaufanya ikiwa Halmashauri...