Thursday, September 15, 2016

DC MUFINDI AIFUNGIA SHULE YA SEKONDARI YA ST. JOSEPH ZADRASS KWA UTAPELI

 Mkuu wa wilaya aliyevalia koti la suti akizungumza na wanafunzi, waliojitambulisha kwamba wao ni kidato cha tatu. 
Mkuu wa wilaya na maofisa wa polisi na halmashauri wakikagua nyaraka shuleni hapo.

Na fredy mgunda,Iringa

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Mh. Jamuhuri William ametoa muda wa siku 07 kwa mkuu wa shule ya sekondari ya St. Joseph Zadrass iliyopo kata ya Rungemba katika kijiji cha Kitelewasi Wilayani Mufindi, awe amerejesha fedha kwa wanafunzi takribani 70 aliowasajili sanjari na kusitisha mpango wa utoaji elimu ya sekondari shuleni hapo baada ya kubaini kuwa mmiliki wa shule hiyo anaendelea kudahili wanafunzi licha ya kufutiwa usajili  miaka nane iliyopita.

Taarifa ya liyotolewa na kitengo cha habari na mawasiliano cha halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, imebainisha kuwa Mkuu wilaya ametoa maagizo hayo mara baada ya kufanya ziara ya kushitukiza shuleni hapo na kuendesha zoezi la ukaguzi wa nyaraka za uhalali na uhai wa shule hiyo.

Mh. William amesema, licha ya shule hiyo kufutiwa usajili mnamo mwaka 2009 kwa kupoteza sifa, bado imeendelea kusajili wanafunzi kwa mtindo wa kuwatapeli kwa ushirikiana na chuo cha uwalimu cha Rungemba kwa hoja ya kuendesha masomo ya ziada kwa wanaotaka kurudia mitihani wakati baadhi ya nyaraka zinaonesha hadi mwaka jana wamepokea wanafunzi waliohamia kutoka shule nyingine ambazo zipo katika mfumo rasmi.

Naagiza, ndani ya wiki moja yaani ifikapo tarehe 20 mwezi huu wanafunzi wote wawe wameondoka, nimemwagiza mkuu wa polisi wilaya na mdhibiti ubora wa elimu kusimamia zoezi hilo na itakapofika tarehe 20 nitafuatilia utekelezaji wa agizo langu hili”

Aidha, Mkuu huyo wa wilaya amewaonya wamiliki wote wa vyuo na shule Wilayani Mufindi Kuhakikisha wanaendesha taasisi zilizosajiliwa  na kuwataka wazazi na walezi kupeleka watoto wao katika shule ambazo zinausajili wa serikali kwani mwisho wa siku watakuwa wamepoteza fedha na Muda wa watoto wao na kusisitiza kuwa akiwa mkuu wa Wilaya hiyo  hatakubali kuona utapeli kama huo unatokea Wilani humo.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More