Thursday, September 29, 2016

ZIMWI LA TEGETA ESCROW LAMTISHA PROFESA TIBAIJUKA, AKATAA KUPOKEA DOLA 300,000 BAADA YA KUPEWA TUZO YA KIMATAIFA

 Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka akionesha tuzo ya kimataifa (UN) ya Maendeleo Endelevu ya Mwana Mfalme Khalifa Bin Salman Al Khalifa aliyotunukiwa hivi karibuni New York Marekani wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo.  Profesa Anna Tibaijuka akionesha cheti alichokabidhiwa sanjari na tuzo hiyo.  Profesa Tibaijuka akisisitiza jambo katika mkutano huo na wanahabari. Kulia ni Mratibu wa mkutano huo, Mussa Ally.  wanahabari wakichukua taarifa hiyo. Mkutano na wanahabari ukiendelea. Na Dotto Mwaibale MBUNGE wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka amekacha kuchukua dola 300,000 alizopewa baada ya kutunukiwa tuzo ya  Maendeleo Endelevu aliyopewa na Umoja wa Mataifa...

MRADI WA URASIMISHAJI ARDHI UBUNGO WAINGIA MIZENGWE WATENDAJI WATISHIA KOGOMA KWA KUKOSA POSHO

Waziri wa Ardhi, William Lukuvi NaFredy Mgunda WATENDAJI na vibarua wanaofanya kazi ya kupima ardhi katika mradi wa urasimishaji wa ardhi katika maeneo yaliyojengwa kiholela katika Kata ya Kimara  wilayani Ubungo umeingia mdudu baada ya kutishia kugoma kutokana na kutolipwa fedha za posho ya kazi hiyo kwa zaidi ya miezi mitatu. Hatua hiyo imefikiwa baana ya kuona baadhi ya vongozi wanaosimamia mradi huo wa kuanza kujinufaisha wenyewe na kuwanyonya watendaji wakiwemo vibarua  hao. Wafanyakazi wa upimaji wa ardhi kutoka wizarani na vibarua hao wakiongea kwa nyakati tofauti na gazeti hili kwa masharti ya kuto andikwa majina yao gazetini  wamesema  viongozi hao kupitia mradi huo wamejenga mazingira ya  kujinufaisha...

MCHUNGAJI DKT.DANIEL KULOLA KURINDIMA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA INJILI JIJINI MWANZA.

Kanisa la EAGT Posta “B” Mabatini Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Lameck Nkumba, linawakaribisha watu wote kwenye mkutano mkubwa wa injili utakaofanyika katika viwanja vya kanisa hilo vinavyotizamana na geti la polisi Mabatini nyuma ya iliyokuwa Orange Tree Hotel. Mhubiri wa kitaifa na kimataifa ambaye amehubiri mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Marekani, Canada, Uingereza, Ireland, Wales , Scotland, Ujerumani, Dernmark, Swirtzland, Afrika Kusini, DRC Congo na mengine mengi, Dkt.Daniel Moses Kulola (pichani), atahudumu kwenye mkutano huo akishirikiana na wahubiri wengine. Ni wiki moja yenye miujiza na uponyaji wa nguvu ya Mungu, kuanzia jumapili tarehe 9.10.2016 hadi jumapili tarehe 16.10. 2016 muda ni kuanzia saa 9.00 mchana hadi saa...

Vijana watakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kuondokana na umaskini

Katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa nchi yenye maendeleo na iliyo na watu ambao wamefanikiwa kimaisha, vijana nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kujikomboa na janga la umaskini lakini pia kulisaidia taifa kupata maendeleo. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri wakati akizungumza na vijana ambao wanajifunza ujasiriamali na kuwambia ni vyema wakaongeza bidii katika ndoto wanazotamani kuzifikia ambazo pia zitawasaidia kuondokana na umaskini ambao umekithiri nchini. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HiTech International, Paul Mashauri akizungumza na vijana kuhusu ujasiriamali. Alisema ili mtu kufanikiwa kimaisha haitaji zaidi elimu ya darasani bali ni muhusika mwenyewe...

SSRA YAWATOA HOFU WANANCHI KUHUSU MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII NCHINI

 Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Onorius Njole (kushoto), akitoa ufafanuzi mbalimbali kwenye semina ya siku moja ya wanahabari kuhusu mifuko ya jamii Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Uhamasishaji, SSRA, Sarah Kibonde.  Mkurugenzi wa Tafiti, Sera na Tathmini wa SSRA, Ansgar Mushi akitoa mada katika warsha hiyo.  Waandishi wa habari wakiwa katika semina hiyo.  Waandishi wakiwa kwenye semina hiyo  Semina ikiendelea.  Waandishi wa habari wakichukua mambo kadhaa kwenye semina hiyo.  Wanahabari wakiwa makini katika semina hiyo.  Maswali yakiulizwa.  Taswira meza kuu katika...

TAARIFA YA KATIBU MKUU JUU YA UPATIKANAJI WA DAWA

...

Wednesday, September 28, 2016

22 Watiwa Mbaroni kwa tuhuma za Kutaka Kuchoma Moto Ofisi za CUF Dar es Salaam

Ikiwa zimepita siku kadhaa tangu Kamati ya Uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) kutuhumu baadhi ya viongozi wake waliosimamishwa uanachama kupanga njama za utekaji viongozi wa chama hicho, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikiliwa wanachama wa CUF 22 kwa tuhuma za kupanga njama za kufanya fujo na kuchoma mali za ofisi za chama hicho. Ikumbukwe kuwa, Septemba 16,2016 CUF kupitia Kurugenzi yake ya Habari na Uenezi ilitoa taarifa ya jaribio la utekaji wa Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha CUF, Joran Bashange ambapo chama hicho kiliwatuhumu Magdalena Sakaya, Abdul Kambaya na Profesa Ibrahim Lipumba kuwa walinzi wao walijaribu kufanya tukio hilo. Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,...

DC KONGWA AMTUMBUA MENEJA WA MAMLAKA YA MAJI

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi akizungumza wakati wa kikao cha Kumng'oa Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na salama Wilyani humo Watumishi wa Mamlaka ya Maji safi na salama WIlayani Kongwa wakizunguza na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Deogratius Ndejem...

Tuesday, September 27, 2016

MAONYESHO YA FILAMU ZA BEIJING 2016 CHACHU KWA UKUAJI WA SANAA NCHINI

 Washindi wa kwanza hadi wa tatu wa mashindano ya sauti waliopatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China wakionesha tuzo baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo. Washiriki 10 walishinda mashindano hayo. Kutoka kushoto ni Hilda Malecela, Safiya Ahmed na Sadiq Kututwa. Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura akisalimiana na mmoja wa washindi 10 wa mashindano ya vipaji vya sauti, Abraham Richard, ambao watakakwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes jijini Beijing, China wakati wa hafla fupi ya Maonyesho...

CHADEMA IRINGA YASAIDIA ZAIDI YA WANAFUNZI MIA MBILI (200) KUENDELEA NA MASOMO

 Diwani wa   viti maalum CHADEMA Sara Mwajeka na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Igumbilo, Fredrick Asenga wakionyesha mfano wa sare za wanafunzi walizotoa msaada  Naibu Meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Igumbilo, Fredrick Asenga wakiwa tayari kukabidhi sare kwa wanafunzi Hawa ni baadhi ya wanafunzi mia mbili (200) wanaoishi katika mazingira magumu wanatarajiwa kusaidiwa msaada wa pesa kwa ajili ya kununulia sabuni,nauli kila wiki na sare za shule ya msingi.   NA FREDY MGUNDA,Iringa ZAIDI ya wanafunzi mia mbili (200) wanaoishi katika mazingira magumu wanatarajiwa kusaidiwa msaada wa pesa kwa ajili ya kununulia sabuni na nauli kila wiki na wanawake walionda...

Page 1 of 69412345Next
Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More