
Matukio
ya kutupa watoto wachanga yameendelea mkoani Morogoro ambapo mtoto
mchanga wa siku moja ameuwa na kutupwa vichakani katika eneo la
kichangani mjini Morogoro.
Mtoto huyo mwenye jinsi ya kike anaonekana ametupwa kwa saa kadhaa
zilizopita ambapo wakizungumzia tukio hilo baadhi ya mashuhuda
wamelalamikia kuongezeka kwa matukio ya watoto wachanga kutupwa ambapo
wameomba wazazi kuwahurumia watoto wasio na hatia huku baadhi ya
wakinamama waliokuwepo katika tukio hilo wameonyesha kusikitishwa na
kueleza wakati mwingine inatokana na baadhi ya wanaume kukwepa majukumu.
Naye mwenyekiti wa mtaa na diwani wa kata ya kichangani John Waziri
walioshuhudia tukio hilo wamesema tukio hilo si la kuvumilika...