Tuesday, February 28, 2017

AZANIA GROUP KUWAKILISHA TANZANIA KATIKA MASHINDANO YA A.MASHARIKI YA STANDARD CHARTERED

Timu ya Azania Group, ndiyo itakayowakilisha Tanzania katika mashindano ya kikanda ya Afrika Mashariki, ya Benki ya “Standard Chartered-Road to Anfield” yatakaofanyika uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park Jumamosi, Machi 4. Azania walipata ushindi huo kwa kuichakaza timu ya H&R Consultancy mabao ya 6-5 kwa penati dhidi ya katika mchezo wa kukata na shoka uliofanyika mwishoni mwa wiki na kufanikiwa kuipeperusha bendera ya Tanzania. Kwa maana hiyo, Azania Group wanatarajia kumenyana uso kwa uso na washindi wa michuano hiyo kutoka nchi za Kenya na Uganda. Washindi wa michuano hiyo nchini Uganda ni timu ya Cocacola wakati kidedea wa kombe hilo nchini Kenya ni Radio ya Capital FM. Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania...

UNESCO KUENDELEA KUSAIDIA REDIO JAMII KUKUZA DEMOKRASIA

Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeahidi kuendelea kuzisaidia redio jamii kwa lengo la kuhakikisha sauti za wanyonge zinapazwa na kusikika ili kukuza demokrasia nchini. Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues alisema UNESCO alisema kuwa wakati umefika kwa wadau wa sekta ya habari kufikiri kwa kina namna ya kuhabarisha umma kwa kuangalia namna ya uwasilishaji ambapo kwa sasa changamoto kubwa ni kasi ya ukuaji wa teknolojia ya habari na namna ambapo redio zinaweza kushindana na vyombo vingine. Alisema kwa wanahabari wanapaswa...

ZOOMTANZANIA.COM YATANGAZA AFISA MTENDAJI MKUU MPYA

Bi Mili Rughani, gwiji katika anga la teknolojia Afrika, akabidhiwa kijiti cha uongozi wa tovuti namba moja ya matangazo Tanzania, ZoomTanzania.com, katika kuendeleza safari ya mafanikio. Miaka ya hivi karibuni imekuwa ya kusisimua sana kwa hii kampuni ya dot-com ya Kitanzania. Mnamo Septemba 2014, Ringier Afrika ilichukuwa asilimia kubwa ya umiliki wa kampuni ya Zoom Tanzania.  Hii iliwezesha upatikanaji wa rasilimali na utaalamu unaohitajika zaidi ili kukua zaidi. Kisha mwaka 2016, ZoomTanzania.com ilikuwa jiwe kuu la msingi katika muungano wa Ringier Africa na One Africa Media, na kufanikisha kuundwa kwa kundi linaloongoza kwa matangazo ya mtandaoni barani Afrika - Ringier One Africa Media (ROAM). "Imekuwa ni safari ya...

BOHARI YA DAWA (MSD) YAPIGA HATUA KUWEZESHA UZALISHAJI DAWA KWA NJIA YA UBIA NA SEKTA BINAFSI (PPP)

 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bwana, Laurean Bwanakunu (kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri  ya Mji wa Kibaha Bi.Jenifa Omolo wakibadilishana hati baada ya kusaini makubaliano ya umilikishwaji wa eneo la ardhi, lenye ukubwa wa mita za mraba 400,000 Dar es Salaam leo, ambayo itatumika kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha kuzalishia dawa na vifaa tiba Kibaha mkoani Pwan...

Monday, February 27, 2017

SAMANI ZA NDANI ZAMNG’ARISHA JACQUELINE NTUYABALIWE KWENYE FORBES

KATIKATI ya foleni katika jiji la Dar es Salaam ndani ya gari nyeupe aina ya Mercedes S550, Jacqueline Ntuyabaliwe, mrembo wa miaka 38, macho yake yalikuwa yametulia katika simu yake ya mkononi. Alikuwa akiangalia seti ya samani za eneo la kulia chakula. Kwa bashasha, baada ya muda kidogo anatanua picha hiyo kisha ananisogezea simu yake ya mkononi kunionesha picha anayoiangalia.  “Hii ni moja ya samani tulizonazo,” anasema huku akinionesha seti hiyo ambayo imetengenezwa na Molocaho by Amorette, kampuni ya kutengeneza samani aliyoianzisha hivi karibuni.  “Samani hizi zimetengenezwa kutokana na mbao zilizotwaliwa kutoka katika mashua za zamani za mizigo kwenye fukwe za Tanzania upande wa bahari ya Hindi,” anasema mjasiriamali...

ZAIDI YA SHILINGI MILIONI NNE ZAPATIKANA KWENYE HARAMBEE ILIFANYWA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA ILEJE

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE MicrosoftInternetExplorer4 /* Style Definitions */ table.MsoNormalTable {mso-style-name:"Table Normal"; mso-tstyle-rowband-size:0; mso-tstyle-colband-size:0; ...

SPIKA MSTAAFU WA ZANZIBAR, PANDU KIFICHO AONGOZA MAHAFALI YA NNE YA CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO (UB), KAWE JIJINI DAR ES SALAAM

Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, akimtunuku Mtihimu wa kwanza wa Falsafa ya Udaktari (PhD), Fadhil Innocent baada ya kuhitimu katika mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo hicho, Kawe jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk. Costa Mahalu. Kificho alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.  Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho (katikati), akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk. Costa Mahalu (kushoto) na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Jaji mstaafu Steven Bwana baada ya kuwasili kwenye mahafali hayo. Mtihimu wa kwanza wa Falsafa ya Udaktari...

Page 1 of 69412345Next
Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More