Meneja wa kanda za nyanda za juu kusini wa mtandao wa simu wa tigo Davis Kisamo akimkabdhi mfano wa hundi ya shilingi milioni tatu wakala wa tigo pesa mkoani Iringa Gypson Chaula na makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za tigo mkoani Iringa
Meneja wa kanda za nyanda za juu kusini wa mtandao wa simu wa tigo DavisKisamo akiwa na wafanyakazi wengine wa tigo pamoja na wakala wa tigo pesa mkoani Iringa Gypson Chaula wakiongea na waandishi wa habari katika ofisi za tigo mkoani Iringa
Na Fredy Mgunda,Iringa.
WAKALA wa tigo pesa mkoani
Iringa Gypson Chaula ameshinda kiasi cha shilingi million tatu (3,000,00) katika promotion ya push inayoratibiwa na
kampuni ya mtandao wa simu wa tigo nyanda za juu kusini.
Akizungumza na waandishi wa
habari meneja wa kanda za juu kusini wa mtandao wa simu wa tigo Davis Kisamo alisema
kuwa wamekuwa wakitoa zawadi mbalimbali kwa mawakala wa mtandao wa tigo
wanaofanya vizuri kwa kuongeza miamala.
“Push promotion inasaidia
kukuza mitaji ya mawakala wanaofanya vizuri kuwahudumia wateja wa kuweka pesa
zao kwa mawakala,hivyo alifanikiwa kushinda ni yule wakala anayefanya miamala
mingini kuliko wakala mwingine” alisema Kisamo
Kisamo alisema kuwa hii ni mara
ya pili kwa mawakala kupata zawadi ya pesa kutoka mtandao wa tigo ili kuwafanya
waipende kazi hii ya kuwa wakala na kuwa na uwezo wa kuwahudumia vizuri wateja
wanapotaka huduma.
“Tunaangalia kuwa wakala kwa
miezi mitatu anafanya nini na ameongeza kiasi gani cha wateja hivyo akifanya
vizuri ni tunawapa zawadi hizi ili kuwaongezea nguvu kwa kutoa huduma bora kwa
wateja wa mtandao wa tigo” alisema Kisamo
Aidha Kisamo Alisema kuwa
promotion hiyo inawahusisha mawakala wote wa nyanda za juu kusini wanatoa
huduma ya mtandao wa tigo na huwa wanapata zawadi mbalimbali kulinga na kufanya
kwake vizuri kwa kuongeza miamala ya tigo pesa
Kisamo alimalizia kwa kuwaomba Tanzania
kuendelea kutumia huduma inayotolewa na mtandao wa simu wa tigo kwa kuwa unatoa
huduma bora ambazo zinasaidia katika maisha ya watanzania wengi.
Naye wakala wa tigo pesa mkoa
wa Iringa Gypson Chaula aliishukuru kampuni ya mtandao wa tigo kwa kuwajali na
kuwakumbuka mawakala kwa kuwapa motisha ambayo inachangia kuongezea mtaji.
“Mimi ninawapongeza sana
viongozi wa mtandao wa tigo nyanda za juu kusini kwa kutujali na kuanzisha
promotion hii ya push kwa kuwa inatuongea mtaji sisi mawakala” alisema Chaula
Chaula aliwataka watanzania
kuendelea kutumia huduma za mtandao wa simu wa tigo kwa kuwa unatoa huduma
nzuri kwa watumiaji wote wa mtandao huu.
0 comments:
Post a Comment