Baadhi
ya Madaktari watoa huduma ya meno na kimywa pamoja na watumishi wa
Fastjet wakiwa wamewasili jijini Mwanza wakitokea Dar es salaam.
Madaktari kutoka
chama cha madaktari wa kinywa na meno Tanzania wakiwa wilayani tarime
mkoa wa mara kuendelea kutoa elimu ya kinywa na meno ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya wiki ya afya ya kinywa na meno Duniani, ambapo walikuwa
wanatoa huduma za uchunguzi,matibabu na elimu kwa wakazi wa wilaya hiyo
ikiwa ni pamoja na kuwafikia wanafunzi na watoto yatima.
Msemaji
wa Fastjet Tanzania Bi. Lucy Mbogoro akiwapatia wanafunzi dawa za
mswaki pamoja na miswaki kwa ajili ya kuendelea kuweka meno yao safi
pamoja na vinywa vyao.
Mmoja wa madakrtari wa meno na kinywa akiendelea kutoa elimu kwa wanafunzi.
Mh. Mariam Mkono,
Diwani wa Viti Maalum akizungumza na madaktari wa kinywa na meno kijijini Nyamwaga.
Debora Magasi,
Muuguzi Mkuu wa hospitali ya Halmashauri ya Wilaya akizungumza na madaktari wa kinywa na meno kijijini Nyamwaga
Mganga Mkuu wa Kinywa na Meno wa Mkoawa
Mara, Dkt Nila Jackson, alisema kati ya Machi 13 hadi 16
mwaka huu madaktari hao walifikia jumla ya wananchi 710 katika kijiji cha
Nyamwaga wakiwemo wanafunzi 510 kutoka shule za msingi saba kijijini humo.
Raiswa
Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania Dkt. Ambege Jack
Mwakatobe,
alitoa wito kwa madaktari wa mikoa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi
angalau mara mbili kwa mwezi ili kuwaongezea ufahamu na uelewa wananchi
juu yausafi wa kinywa.
SHIRIKA
la Ndege la Fastjet limewezesha Madaktari wa kinywa na meno kusafiri
kwenda kutoa huduma ya afya ya kinywa na meno bure kwa wananchi wa
wilaya ni Tarime mkoani
Mara.
Madaktari
kutokachama
cha madaktari wa kinywa na meno Tanzania wameanza ziara ya kujitolea
katika wilaya ya Tarime mkoani mara ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
wiki ya afya ya kinywa na meno duniani ambapo watatoa huduma
zauchunguzi,
matibabu na elimu kwa wakazi wa wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kuwafikia
wanafunzi na watoto yatima.
Akizungumza
hivi karibuni wilayani Tarime, Daktari wa Meno wa Wilaya ya Ngara
mkoani Kagera,
Dk. David Mapunda, alisema ziara hiyo itawapatia fursa madaktari hao
kufanya uchunguzi wa kinywa pamoja na kutoa huduma za matibabu pamoja na
elimu kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Alisema
miongoni mwa magonjwa yanayosumbua katika kinywa ni pamoja nakuoza kwa
meno na ugonjwa wa fizi ambayo yanasababishwa na uchafu unaotokana na
kutokupiga mswaki,
kukosea kupiga mswaki au kutumia mswakiusio faa.
Alisema
ili wananchi waepukane na magonjwa hayo ya meno wanapaswa kupiga mswaki
angalau mara mbili kwa siku na kujenga utaratibu wa kuangalia afya ya
kinywa na meno mara kwa mara.
Kwa upande
wake Mganga Mkuu wa Kinywa na Meno wa Mkoawa Mara, Dkt Nila Jackson, alisema kati ya Machi13
hadi 16 mwaka huu madaktari hao walifikia jumla ya wananchi 710 katika kijiji cha Nyamwaga wakiwemo wanafunzi
510 kutoka shule zamsingi saba kijijini humo.
"Kati
ya tarehe hizo Madaktari hao walitoa uchunguzi,
matibabu na elimu ya afya ya kinywa na meno na kati ya tarehe 17 hadi 20
watakuwa katika wilaya ya Tarime na Rorya kuendelea na zoezi hilo," aliongeza Dk.Jackson
Naye
Raiswa
Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (Tanzania Dental
Association), Dkt.
Ambege Jack Mwakatobe, alitaja kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya kinywa
na meno Duniani inayosema
“Sema ah, fikiri akinywa, fikiria afya”
ambayo inalenga kuwahamasisha wananchi kuzingatia afya ya kinywa na meno
ilikujikinga na magonjwa yanayohusiana na ugonjwa wa meno ikiwemo
magonjwa yakisukari na mengine.
Aidha
alitoa wito kwa madaktari wa mikoa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi
angalau mara mbili kwa mwezi ili kuwaongezea ufahamu na uelewa wananchi
juu ya usafi wa kinywa.
Akizungumza kutoka kijiji
cha Nyamwaga, Msemaji wafastjet nchini, Lucy Mbogoro, alisema shirika la
fastjet linafuraha kuwa sehemu ya shughuli hii inayofanywa na madaktari hawa wazalendo.
"Shirika
la fastjet limewawezesha madaktari hawa kusafirikutoka Dar es salaam hadi Mwanza na kurudi ikiwa ni sehemu yampango
wake wakurudisha shukrani kwajamii," alisema.
0 comments:
Post a Comment