Mjumbe wa halmashauri kuu ya
taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas amempongeza mbunge wa viti
maalum mkoa wa Iringa Rose Tweve kwa kuinua uchumi wa wananchi kwa kutoa kiasi
cha shilingi laki sita (600,000) kwa kata kumi na saba za wilaya ya
Mufindi mkoani Iringa.
Mbunge wa viti
maalum mkoa wa Iringakupitia chama cha mapinduzi Rose Tweve akiongea mbele ya baraza kwa kuonyesha furaha yake mbele ya mjumbe wa halmashauri kuu ya
taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas baada ya kuambiwa kuwa ataongezewa shilingi milioni kumi na nane kwa ajili ya maendeleo ya akina wanawake wa wilaya ya Mufindi
viongozi mbalimbali na wabunge wa viti maalum walihudhuria baraza hilo.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MJUMBE wa halmashauri kuu ya
taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas amempongeza mbunge wa viti
maalum mkoa wa Iringa Rose Tweve kwa kuinua uchumi wa wananchi kwa kutoa kiasi
cha shilingi laki sita (600,000) kwa kata kumi na saba za wilaya ya
Mufindi mkoani Iringa.
Akingumza wakati wa baraza la
UWT wilaya ya Mufindi Salim Asas alisema kuwa amefurahishwa na mkakati mbunge Rose
Tweve kwa kufanikiwa kuwafikia wananchi wa kipato cha chini kabisa ambao ndio
wanastahili kuinuliwa kiuchumi kuliko wananchi ambao tayari wanauchumi mkubwa.
“Kwa kweli niwe muwazi kuwa
nimefurahishwa na hiki kitu ambacho huyu mbunge anakifanya kwa kuwawezesha
wananchi ambao ndio serikali ya awamu ya tano inataka kuwafikia na kuwainua
kiuchumi” alisema Asas
Asas aliwata wabunge wengine
kuiga mfano wa mbunge Tweve kwa kazi anayoifanya ya kuwawezesha akina mama na
wananchi wengi kwa kuwa hiyo ndio inakuwa faida kwa taifa.
“Naombeni wabunge wangu wote
tufanye kazi kama anayoifanya mbunge Rose Tweve kwa kuwafikia wananchi wa chini
ambao mara nyingi imekuwa vigumu kuwafikia kutokana na sababu mbalimbali”
alisema Asas
Aidha Asas alisema kutokana
kazi kubwaanayoifanya mbunge Rose Tweve atachangia kiasi cha shilingi laki tano
(500,000) kwa kila kata kwa kata zote 36 za wilaya ya Mufindi ambapo atatoa
kiasi cha shilingi milioni kumi na nane (18,000,000) kwa ajili ya kuchangia
vikundi hivyo.
Kwa hili sipepesi macho
nampongeza sana mbunge Rose Tweve kwa kazi kubwa anayoifanya kuhakikisha
wanawake wanapata mafanikio kwa kuwawezesha kama alivyofanya kwa kufanya hivyo
amefanikiwa kuwafikia wanawake walio na kipatao cha chini kabisa na nitaendelea
kukusaidia mbunge kwa kazi unazozifanya kwa ajili ya maendeleo” alisema Asas
Kwa upande wake katibu wa UWT
wilaya ya Mufindi Mwanaidi Kaleghela alimshikuru MNEC Salim Asas kwa kutoa
msaada mkubwa kama huo ambao hata wao hawakutegemea kutokea kitu kama
hicho,ukipiga mahesabu utagundua kuwa ametoa milioni ishirini na nne kwa UWT
mufindi.
Kaleghela alisema hadi kufika
sasa mtaji umekuwa hadi kufikia shilingi milioni hamsini na mbili laki tano (52,500,000)
na fedha hizo zinasimamiwa na umoja wa wanawake wilaya ya Mufindi (UWT)
Bila mchango wa mbunge Rose
Tweve tusingeweza kuwafikia wananchi kwa kiasi hiki hivyo nachukua nafasi hii
pia kumpongeza mbunge wetu kwa kazi anazozifanya kwa maendeleo ya wananchi.
Kwa upande wake mbunge Rose
Tweve alikuwa ni mtu mwenye furaha baada ya kupokea hongera na kuchangiwa kiasi
cha shilingi milioni kumi na nane (18,000,000) kutoka kwa MNEC.
“Mnaniona nabubujika machozi
kutokana na furaha niliyonayo kutoka na mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya
chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Salimu Asas kutambua mchango wangu” alisema
Tweve
0 comments:
Post a Comment