Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati leo ametembelea kambi ya timu ya Panama Girls kwa kutoa amasa na zawadi kwa ajili ya kuwaongezea nguvu katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Kigoma Sisters ya mkoani Kigoma.
Meneja wa uwanja wa ndege wa Nduli Anna Kibopile aliwapongeza timu hiyo kwa kuwa na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu tofauti na timu nyingine za wanawake na kuahidi kununua kila goli kwa kiasi cha shilingi elfu kumi katika mchezo wa kesho.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwakabidhi msaada wa vyakula alivyowapelekea hii leo
Baadhi ya wacheza wa timu ya Panama Girls ya mkoani Iringa walipokuwa wanamsikiliza mbunge Ritta Kabati na viongozi wengine walipotembelea kambini hii leo
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati
leo ametembelea kambi ya timu ya Panama Girls kwa kutoa amasa na zawadi kwa
ajili ya kuwaongezea nguvu katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Kigoma Sisters
ya mkoani Kigoma.
Akizungumza
katika kambi ya timu hiyo iliyopo eneo sabasaba Mbunge Kabati alisema kuwa
anaipenda timu ya Panama kutokana na kuwa na wachezaji wa vipaji vya hali ya
juu na ndio maana kila mwaka amekuwa akiichangia chochote alichonacho.
“Naomba
kukiri kuwa mwaka huu sijaja kabisa nah ii ndio mara yangu ya kwanza kuja
kuitembelea timu hivyo nahitaji kufunza vitu viti kutoka kwenu na kwa viongozi
ili nikitoka hata nikavifanyie kazi kama nilivyofanya mwaka jana” alisema
Kabati
Kabati
akisema kuwa amewaletea vyakula kwa ajili ya kuongeza nguvu kwani mwanamichezo
akila vizuri ndio atafanya vizuri hata uwanjani.
“Mnajua
kuwa msipokula vizuri itakuwa ngumu sana kucheza uwanjani na mkapata ushindi
hivyo nimeanza na kuletaa chakula hiki kasha nitazikuchukua changamoto zenu na
kwenda kuzitafutia ufumbuzi” alisema Kabati
Aidha
Kabati alisema kuwa atanunua kila goli litakalofungwa siku ya kesho kwa kiasi
cha shilingi elfu ishirini na pesa hiyo itakuwa kwa matumizi ya wachezaji wote
na kuwaomba kucheza kwa kujituma na kuhakikisha kesho wanapata ushindi wa
kishindo ili kusahau machungu ya mechi ilipita.
Kwa
upande wake meneja wa uwanja wa ndege wa Nduli Anna Kibopile aliwapongeza timu
hiyo kwa kuwa na wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu tofauti na timu
nyingine za wanawake na kuahidi kununua kila goli kwa kiasi cha shilingi elfu
kumi katika mchezo wa kesho.
“Mimi
nitanunua kila goli kwa shilingi elfu kumi hivyo naomba kesho fungeni magoli
mengi ili pesa initoke nyingi kwa kuwa naipenda sana hii timu” alisema Kibopile
Naye
makamu wenyekiti Mwanaheri Kalolo alimshukuru mbunge huyo kwa kujitolea mara
kwa mara kuisaidia timu hiyo na kumuomba awatafutie wadau wengine wanaoweza
kuisaidia timu hiyo kwa kuwa timu hiyo inauhitaji mkubwa wa pesa.
0 comments:
Post a Comment