Katibu wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT)
Mkoa wa Iringa Chiku Masanja akiwa mwenyekiti
wa UWT wilaya ya Iringa Ashura Jongo na katibu wa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati wakati walipowatembelea watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga nje kidogo ya manispaa ya Iringa kwa kuwafariji na kutoa msaada Katibu wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT)
Mkoa wa Iringa Chiku Masanja akiwa mwenyekiti
wa UWT wilaya ya Iringa Ashura Jongo,katibu wa mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati pamoja katibu wa umoja wa vijana mkoa wa Iringa (UVCCM) Mgego
Wadau mbalimbli pamoja na watoto yatima wakiwa wanasikiliza maneno ya kufariji kutoka kwa Katibu wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT)
Mkoa wa Iringa Chiku Masanja
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Yatima wanaoishi katika kituo cha Tosamaganga mkoani
Iringa wamepata neema kutoka kwa katibu wa umoja wa wanawake Tanzania (UWT)
Mkoa wa Iringa Chiku Masanja akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali ambao
walifika kituoni hapo kutoa msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya sikuku ya
pasaka kwa watoto hao.
Akiongea
na waandishi wa habari kuhusu hatua hiyo ya kutoa msaada kwa watoto wanaokaa
mazingira magumu, Masanja alisema kuwa lengo lao kubwa ni
kujikwamua kwenye mazingira magumu na ikiwezekana kusiwepo kabisa na watoto
tegemezi.
“Lengo
letu kuu nikujikwamua kutoka kwenye mazingira magumu na kufuta kabisa uwepo wa
watoto tegemezi kwenye jamii yetu” alisema Masenza
Aidha
katibu Masanja alisema kuwa wanafanya hivyo kwa sababu watoto yatima wanaoishi
kwenye mazingira yanayoonekana na yanayoizunguka jamii hivyo itapelekea wao
kuondokana na upweke na kujisikia furaha kama watoto wengine wanaoishi
mazingira ya kawaida.
Masanja alisema kuwa wameguswa kutoa msaada
katika kituo hicho kwa kutenda matendo ya huruma wakati wa kipindi hiki
cha sikuku ya Pasaka kwa watoto kwa kuwa wanamahitiji mengi pia ni kuwapunguzia
ugumu wa maisha walezi wa watoto hao.
Mwenyekiti
wa UWT wilaya ya Iringa Ashura Jongo alisema jamii inapaswa kuwajali yatima na
wanyonge.
Jongo
alisema watanzania ni jamii ya watu wanaopendana hivyo, watoto hao wanapaswa
kuangaliwa kwa hali na mali ili wasihisi upweke wa kuwakosa wazazi wanapaswa
kuangaliwa kwa jicho la tatu kwani hao ni wanyonge.
Lakini
Jongo alisema inampasa kila mmoja kwa wakati wake kurudi mwenyewe na kuangalia
namna ya kuwasaidia watoto hao wanyonge, kwani nao wanahitaji upendo na misaada
mingine kama watoto wenye kulelewa na baba na mama
Nae
Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Tosamaganga amewashukuru viongozi
wote,wananchi wote pamoja na mkuu wa mkoa kwa kuwaona kwa jicho la pekee na
kwenda kuwapa msaada katika kituo hicho.
0 comments:
Post a Comment