Wednesday, March 7, 2018

WAZIRI UMMY MWALIMU ARIDHISHWA NA UTENGAJI KAZI WA VIONGOZI WA HALMASHAURI YA ILEJE

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi pamoja na mkuu wa wilaya hiyo Joseph Mkudew wakielekea eneo ambalo kituo cha afya kinajengwa kwa ajili ya kwenda kufanya ukaguzi na kupokea maelezo ya ujenzi huo na namna pesa za serikali katika sekta ya afya zinavyotumika.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi   pamoja na viongozi wengine wa wilaya hiyo wakiwa kwenye eneo ambalo kituo hicho kinajengwa.
 Mkurugenzi mtendaji wa halmashuri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akifanya kazi kwa vitenda wakati wa ziara ya waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ya ukaguzi miradi ya afya na kujua namna gani pesa zilizotolewa na serikali zinavyotumika katika halmashauri ya wilaya ya Ileje

Na Fredy Mgunda,Ileje

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amefanya ziara ya ukaguzi miradi ya afya na kujua namna gani pesa zilizotolewa na serikali zinavyotumika katika halmashauri ya wilaya ya Ileje mkoani Songwe.
 
Akiwa katika zira hiyo,Waziri Mwalimu alifanikiwa kukagua kituo cha afya cha Lubanda ambacho kilipewa kiasi cha shilingi milioni mia tano(500)  kutoka serikalini kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya kwa wananchi wa halmashauri hiyo.

“Mimi nimekuja kuangalia utekelezaji wa pesa ambazo serikali tunazileta huku kwa kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya,maana kumekuwa na watendaji ambao wamekuwa wakizitumia vibaya pesa ambazo tumekuwa tukizileta huku” alisema  Waziri Mwalimu

Waziri Mwalimu alisema kuwa ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa kituo cha afya cha Lubada unaoendelea kwa kasi nzuri na kwa viwango ambavyo serikali inavitaka na kuahidi kuwa ukimalika ujenzi huo utawaletea gari la kubebea wagonjwa (ambulance) kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania.

“Kwa hapa mlipofikia nawapongeza sana kwa kuwa kazi nimeiona kwa macho yangu mwenyewe hivyo mkimaliza ujenzi nitakikisha kila kitu kinachotakiwa hapa kitakuwepo ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa wilaya ya Ileje” alisema Waziri Mwalimu

Hata Waziri Mwalimu aliupongeza uongozi wa halmashauri ya Ileje kwa kufikisha asilimia tisini na moja (91) ya wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ambao unarahisisha upatikanaji wa huduma bora ya afya kwa wananchi wanaotumia mfuko huo.

“Niwapongeze tena kwa kazi kubwa mliyofika ya wananchi wengi kukubali kujiunga kwenye mfuko huo,maana kuna halmashauri nyingine zijafgika hata robo yenu hiyo naona utendaji wenu uliotukuka katika kuwatumikia wananchi wa Ileje” alisema Waziri Mwalimu

Waziri Mwalimu alizitaka halmashauri nyingine kuiga mfano wa halmashauri ya ileje kwa namna wanavyofanya kazi kwa ushirikiano mkubwa baina ya mkurungezi mtendaji na mkuu wa wilaya hiyo ndio maana kuna matokeo chanya.

“Nichuke nafasi hii kukupongeza sana mkurugezi wangu Haji Mnasi na mkuu wa wilaya Joseph Mkude kwa ushirikiano mnaoushesha katika kuleta maendeleo kwa wananchi wa wilaya ya Ileje,napenda kama halmashauri zote hapa nchini zingekuwa kama halmashauri yetu tungekuwa tumefika mbali kimaendeleo” alisema Waziri Mwalimu

Awali akisoma hotuba kwa waziri, mkurugenzi wa halmashuri hiyo Haji Mnasi alisema kuwa halmashauri imejiwekea mikakati ya kuhakikisha wananchi wote wanajiunga na mfuko wa afya ya jamii  kwa kutoa elimu juu ya umuhimu wa kujiunga kwenye mfuko huo.

“Tunasheria ya mwaka 2004 ambayo inawataka wananchi wote wajiunge kwenye mfuko huo hivyo tutaitumia vizuri sheria hiyo kuhakikisha kuwa kila mwananchi anajiunga kwenye mfuko huo akiwa tayari amepatiwa elimu ya kutosha na kumfanya ajiunge mwenyewe bila kulazimishwa” alisema Mnasi

Mnasi alisema kuwa huduma za matibabu kwa wazee zinatolewa katika vituo vyote 33 vya huduma za afya na jumla ya wazee 11463 waliotambuliwa na walipewa vitambulisho ni 8954 sawa na asilimia 78 ambapo jumla ya shilingi 7,196,000 zilitumika mwaka 2016/2017 kwa ajili ya kutoa huduma kwa wazee.

“Lakini ukiangalia mwaka 2017/2018 tumetenga kiasi cha shilingi 28,000,000/= ambapo kwa kila zahanati tunapeleka kiasi cha shilingi 1,000,000 na kwenye vituo vya afya tunapeleka 2,000,000 kwa ajili ya huduma ya wazee na kazi ya kuendelea kuwatambua ni endelevu” alisema Mnasi

Mnasi alimuahidi Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kuwa pesa zote zinazoletwa kutoka kwenye wizara yake zitatumika kama zilivyopangwa na kuhakikisha zinasimamiwa vizuri kama ambavyo wamekuwa wakisimamia pesa zote za serikali zitumike kwa malengo yanayokusudiwa.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More