Tuesday, March 20, 2018

KATIBU RIZIKI KINGUNDE AWATAKA WANAWAKE KUACHANA NA UTEGEMEZI

Katibu wa organization wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (CCM) taifa Riziki Kingunde  akitoa somo kwa wanawake wa kata ya Mkwawa manispaa ya Iringa mkoani Iringa wakati wa ziara ya viongozi wa UWT taifa 
Baadhi ya wanawake na wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Mkwawa wakimsikiliza kwa umakini katibu wa organization wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (CCM) taifa Riziki Kingunde  akitoa somo kwa wanawake wa kata ya Mkwawa manispaa ya Iringa mkoani Iringa wakati wa ziara ya viongozi wa UWT taifa

Na Fredy Mgunda,Iringa.

KATIBU wa organization wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (CCM) taifa Riziki Kingunde amewataka wanawake kote nchini kujikwamua kiuchumi kwa kufanya shughuli ndogo ndogo za ujasiriliamali ili kuachana na utegemezi.

Kingunde alisema kuwa baadhi ya wanawake hasa wa vijiji wamekuwa wakipata msongo wa mawazo kutokana na kutokuwa na kipato licha ya kushiriki shuhuli za uzalishaji mali ngazi ya familia lakini wengi wao wamekuwa hawashirikishwi katika matumizi ya kipato walichokitolea jasho. 

Akizungumza wakati wa ziara ya viongozi wa ngazi za juu wa UWT taifa mkoani Iringa, Kingunde alisema imefika wakati sasa wanawake kusimama kwa miguu yake na kuachana na utegemezi.

Kingundealisema kuwa kuna mifuko maalumu ya kuwaisidia wanawake hasa wa hali ya chini kwa kuwapatia mitaji kupitia vikundi ili kuanzisha biashara ndogo ndogo na kuachana na utegemezi hivyo msaada walioupata utawafanya wapige hatua kubwa zaidi.

Kingunde alisema kuwa kumsaidia mwanamke wa hali ya chini kwa kumuwezesha kimtaji ni kukomboa jamii kwani mama huyo ataweza kuhuduma familia yake bila ya kuwa tegemezi.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alipongeza jitihada zinazofanywa na serikali kwa kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutoa mitaji yenye riba ndogo.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More