Mawaziri
wakuu wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye amehudhuria katika
Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kufuatilia hatma ya kesi ya viongozi 6
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) wakiongozwa na
Mwenyekiti Freeman Mbowe kama watapata dhamana au wataendelea kusota
rumande.
Viongozi
waandamizi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)wamefikishwa
mahakamani leo saa 2 asubuhi katika Mahakama ya Kisutu kwa ajili ya
kusikiliza uamuzi wa dhamana yao huku wakisindikizwa na baadhi ya
wajumbe wa Kamati kuu CHADEMA.
Kesi
hiyo ya Viongozi wa CHADEMA inatarajiwa kutajwa leo chini ya Hakimu
Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambaye anatarajiwa kutoa uamuzi kuhusu
dhamana ya washtakiwa hao.
Hata
hivyo baadhi ya Viongozi wengine wa chama hicho wamefika mahakamani
hapo ili kuwasindikiza viongozi wenzao wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati
Kuu CHADEMA, Edward Lowassa, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Profesa
Abdallah Safari na baadhi ya Wabunge.
0 comments:
Post a Comment