Mkurugenzi
wa halmashauri ya Ileje Haji Mnasi akiwa na viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje wakiongea na mmoja ya wananchi kujua zoezi la uandikishaji wakazi linaendeleaje na kujua changamoto kutoka kwa wananchi.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya Ileje Haji Mnasi akiwa na viongozi wa halmashauri ya
wilaya ya Ileje wakiongea na wananchi kujua zoezi la
uandikishaji wakazi linaendeleaje na kujua changamoto kutoka kwa
wananchi juu ya zoezi hilo.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya Ileje Haji Mnasi akiwa na viongozi wa halmashauri ya
wilaya ya Ileje wakiwa kwenye moja ya ofisi ambayo inahusika moja kwa moja kwenye zoezi la uandikishaji wa wakazi
Mkurugenzi
wa halmashauri ya Ileje Haji Mnasi akiwa na viongozi wa halmashauri ya
wilaya ya Ileje wakiongea na wananchi kujua zoezi la
uandikishaji wakazi linaendeleaje na kujua changamoto kutoka kwa
wananchi na kufurahia mambo kadhaa kutoka kwa wananchi.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya Ileje Haji Mnasi akiwa na viongozi wa halmashauri ya
wilaya ya Ileje wakifurahia hali ya hewa ya halmashauri hiyo
Na Fredy Mgunda,Iringa.
UONGOZI wa Halmashauri ya Wilaya
ya Ileje Mkoani Songwe umeanza kufanya tathimini ya kujua wakazi wangapi
wameandikishwa kwa njia ya eletroniki (ePRS) kwa lengo la kutaka kutambua kuwa
wilaya hiyo inawakazi wangapi wanaoishi eneo hilo.
Akizungumza na blog hii mkurugenzi
wa halmashauri ya Ileje Haji Mnasi alisema wameamua kufanya tathimini hiyo
baada ya kubaini kuwa wafanyakazi wengi wa umma hawajaandikishwa hivyo
wanatakiwa kupitiwa kwenye kaya zao na kuwaandikisha ili kupata idadi kamili ya
wakazi wa wilaya ya Ileje.
“Taarifa za awali zinaonyesha
kuwa watumishi wa umma hawajajiandikisha kwenye zoezi hili hivyo nawaagiza
waandikishaji kuanzia sasa wahakikishe wanawapitia kwenye kaya zao na
kuwaandkisha ili tujue idadi kamili ya wazi waliopo” alisema Mnasi
Mnasi alisema kuwa
waandikishaji wote wanatakiwa wahakikishe wanaandaa taarifa iliyokamilika na
kuiwakilisha kwa mtendaji wa kata kwa lengo la kuunganisha taarifa za kata yote
na kuziwakilisha kwa mkurugenzi mtendaji wa wilaya.
“Watendaji wa vijiji (VEO’S)
hakikisheni mnaanda taarifa hii na kuiwakilishakwa mtendaji wa kata (WEO’S) ili
aweze kuunganisha na kuwakilisha kwa ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya
Ileje” alisema Mnasi
Mnasi alisema kuwa ukijua idadi
ya wakazi wa eneo husika inasaidia kupanga mipangilio ya kufanya maendeleo na
kuwaletea maendeleo wananchi wa maeneo husika
“Nikwambie mwandishi wa habari
ukijua idadi ya wakazi inakurahisihia hata kuandaa mpango kabambe wa hlmashauri
yako tofauti na kufanya kazi huku ukiwa hujui idadi ya wakazi wako itakuletea
shida sana kupata maendeleo ya haraka” alisema Mnasi
Mnasi alisema kuwa ili
kufanikisha zoezi hili amewaomba wadau mbalimbali,wenyeviti wa vijiji,watendaji
na wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha zoezi hili.
“Bila kupata ushirikiano kutoka
kwa viongozi na wananchi wa ngazi ya kijiji hadi kata wasipotoa ushirikiano
basi zoezi hili litagonga mwamba” alisema Mnasi
Mnasi alimalizia kwa kusema
kuwa zoezi hilo linaendelea katika kata zote za halmashauri ya wilaya ya Ileje
mkoani Songwe
0 comments:
Post a Comment