Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masnza
na viongozi mbalimbali wameanza kusherekea mapema ya Pasaka kwa kutoa msaada wa
chakula na viu mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Watoto Yatima
Tosamaganga, nje kidogo ya manispaa ya Iringa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masnza
na viongozi mbalimbali wakikabidhi mbuzi katika kituo cha Watoto Yatima
Tosamaganga, nje kidogo ya manispaa ya Iringa.
Wadau mbalimbali waliojitokeza kutoa zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga, nje kidogo ya manispaa ya Iringa.
Viongozi mbalimbali wa serikali waliojitokeza kutoa zawadi kwa watoto yatima wa kituo cha Tosamaganga, nje kidogo ya manispaa ya Iringa.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza
na viongozi mbalimbali wameanza kusherekea mapema ya Pasaka kwa kutoa msaada wa
chakula na viu mbalimbali kwa watoto wanaolelewa katika kituo cha Watoto Yatima
Tosamaganga, nje kidogo ya manispaa ya Iringa.
Watoto hao kwa mujibu wa Kaimu Mkuu
wa Kituo hicho, Sista Winfrida Mhongole, ni wale waliopoteza mama zao wakati
wakizaliwa.
“Kituo kinapokea watoto wenye umri
wa siku moja na kuendelea na tunaishi nao hapa kwa miaka saba kabla
hatujawarudisha kwa ndugu zao waliowaleta,” alisema Sista Mhongole.
Pamoja na chakula hicho
kilichojumuisha mchele, mbogamboga, mafuta ya kula na mbuzi, mkuu wa mkoa
Masenza na viongozi wengine waliwapa watoto wanaoishi kituoni hapo zawadi
zingine zilizojumuisha pipi na mafuta ya kupaka na kiasi cha zaidi ya shilingi
lakini nne ambazo zilichangwa na wadau waliofika katika kituo hicho.
Masenza alisema kuwa ofisi yake inatambua
umuhimu wa dhana ya maendeleo shirikishi na ndio maana wamekuwa wakijitolea
kusaidia kuchangia shughuli zingine za kibinadamu mara kwa mara wanapopata
fursa.
“Tulichotoa ni kidogo, lakini
tunaamini kimesaidia kuwapa watoto hawa faraja na kujiona sawa na watoto wenzao
waliopo majumbani kwao,”alisema.
Akishukuru kwa msaada huo, Sista
Mhongole alisema mbali na watoto hao waliopo kituoni hapo, kituo kina watoto
wengine katika shule mbalimbali za msingi, sekondari na vyuo ambazo kwa ujumla
wake kinafanya kituo kiwe na jumla ya watoto 280.
Alisema watoto hao wamepokelewa
kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo ya Iringa, Mbeya, Njombe, Morogoro, Dar es
Salaam na Morogoro.
“Mbali na mapato yatokanayo na
shughuli za kilimo tunazozifanya kama kituo, kituo hiki kinaendeshwa kwa
michango ya wahisani mbalimbali wa ndani na nje. Kwa kweli hatuna wafadhili wa
kudumu,” alisema na kuomba wahisani waendelee kujitokeza kuwasaidia.
0 comments:
Post a Comment