Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wanawake wa benk ya NMB tawi la Mkwawa mkoani Iringa wakishereskea maadhimisho ya siku ya wanawake dunia
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta
Kabati akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wanaume wa benk ya
NMB tawi la Mkwawa mkoani Iringa wakishereskea maadhimisho ya siku ya
wanawake dunia
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta
Kabati akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wanawake wa benk ya
NMB tawi la Mkwawa mkoani Iringa wakishereskea maadhimisho ya siku ya
wanawake dunia na kukata keki ya pamoja
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta
Kabati kilishwa keki na mmoja wa wafanyakzi wa benk ya NMB tawi la Mkwawa mkoani Iringa
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta
Kabati akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakzi wa benk ya
NMB tawi la Mkwawa mkoani Iringa wakishereskea maadhimisho ya siku ya
wanawake dunia
Na Fredy
Mgunda,Iringa.
MBUNGE
wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati
amewataka wanawake mkoani iringa kujifunza kujitegemea katika maisha kutokana
na benk nyingi kutoa mikopo yenye riba ndogo ambayo inawasidia kuwainua
kiuchumi.
Akizungumza
na wafanyakazi wa benk ya NMB tawi la mkwawa Kabati alisema kuwa benk hiyo
imesaidia kuinua maisha ya wanawake kwa kuwawezesha mitaji ya kufanyia biashara
mbalimbali.
“Mimi
nimeshuhudia mara kwa mara mkiviwezesha vikundi vingi vya wanawake ambavyo
mmesaidia kukuza maendeleo ya wanawake wa mkoa wa Iringa na ndio maana wanawake
wengi wamekuwa wakitoa ushuhuda mzuri juu ya huduma za nzuri za benk hii”
alisema Kabati
Kabati
alisema kuwa wanawake wanatakiwa kuwa nguzo ya uchumi kwa kuwa serikali ya
awamu ya tano inataka nchi kuwa ya viwanda hivyo wanawake wasiogope kukopa
kwenye benk ya NMB kwa kuwa inamashariti nafuu.
“Tunaelekea
kwenye uchumi wa viwanda hivyo wanawake tunapaswa kushikamana kwenye uchumi wa
viwanda kwa kuwa benk ya NMB inasaidia maendeleo ya wanawake kwa kuwawezesha
mitaji ya kufania maendeleo” alisema Kabati
Aidha
Kabati amewataka wanawake kuanzisha viwanda vidogo vidogo ambavyo vitasaidia
kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa kuwa benk ya NMB imekuwa ikitoa mikopo ya
kufanikisha wajasiliamali kuanzisha viwanda.
“Hata
saizi ukitaka wajasiliamali waje kwenye kazi furani utakuta wanawake wamekuja
kwa wingi kwa kuwa kwasasa wanawake ndio wanafanya biashara ndogo ndogo hivyo
wanawake wanaweza kufanya biashara yoyote” alisema Kabati
Kabati
aliwataka wanawake kufanya kazi zaidi ya moja ili kuinua na kujiletea maendeleo
na kuondokana na kuwa tegemezi kwa wanaume.
Naye
meneja wa benk ya NMB tawi la mkwawa George Mwita alisema kuwa bank hiyo
imekuwa ikiwawaezesha wanawake kwa kuwapatie elimu ya ujasiliamali na kuwapatia
mikopo yenye riba ndogo.
“Sisi
kama NMB benk tumekuwa tukifanya kazi kwa ukaribu sana na wanawake kwa kuwa
tunajua wanauwezo mkubwa wakufanya biashara ndogo ndogo na zile kubwa” alisema
Mwita
Mwita
aliwataka wanawake kufika kwenye benk ya NMB ili kujua huduma ambazo zinatolewa
na benk hiyo ambayo ipo kila mahali kwa ajili ya kukuza uchumi wa wanawake na
wanaume kwa kuwa benk hiyo haichagui mtu bali inawawezesha wananchi wote.
Ukija
hapa benk ya NMB utapata huduma bora ambayo itakusaidia kuinua uchumi wako na
kuleta maendeleo kwa kuwa tunatoa mikopo mbalimbali yenye mashariti nafuu na
riba yetu sio kubwa” alisema Mwita
0 comments:
Post a Comment